` MIJADALA YA CATA KUWA CHACHU YA KUBORESHA ZAIDI HUDUMA ZA KODI TANZANIA – CG MWENDA

WANDAMAN HOTEL

MIJADALA YA CATA KUWA CHACHU YA KUBORESHA ZAIDI HUDUMA ZA KODI TANZANIA – CG MWENDA

 

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Yusuph Juma Mwenda, amesema mijadala ya Mkutano wa 46 wa Chama cha Wasimamizi wa Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA) itakuwa chachu ya kuboresha zaidi huduma za kodi nchini. Ameyasema hayo leo, Oktoba 7, 2026, wakati akiongoza ujumbe wa CATA katika ziara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) jijini Arusha, ambapo wajumbe wamejifunza matumizi ya teknolojia, ubadilishanaji wa taarifa na mifumo ya Forodha.

Katibu Mkuu wa EAC, Balozi Stephen Mbundi, ameipongeza TRA kwa maandalizi mazuri ya Mkutano wa 46 wa CATA na kusisitiza umuhimu wa teknolojia, ubadilishanaji wa taarifa na uunganishaji wa mifumo katika kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kurahisisha biashara.

Rais wa CATA, Dkt. Abu Tariq Jamaluddin, amesema teknolojia na ubunifu ni muhimu katika kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato na kuboresha huduma kwa walipakodi. Ameipongeza Tanzania kupitia TRA kwa kuendelea kuboresha mifumo ya kodi na kurahisisha ulipaji wa kodi.

Bw. Mwenda amesema TRA itaendelea kutumia maarifa na uzoefu unaopatikana kupitia CATA kuboresha huduma kwa walipakodi, kurahisisha ulipaji wa kodi na kuongeza ufanisi wa ukusanyaji wa mapato kwa maendeleo ya Taifa. Mkutano huo unaendelea jijini Arusha hadi Oktoba 9, 2026, ukiwa na kaulimbiu “Leveraging Technology for Efficient Revenue Collection.”

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464