` MAHAFALI YA DARASA LA SABA KOM YAFANA, WAHITIMU WAPEWA NASAHA

WANDAMAN HOTEL

MAHAFALI YA DARASA LA SABA KOM YAFANA, WAHITIMU WAPEWA NASAHA

 


MAHAFALI YA DARASA LA SABA KOM YAFANA, WAHITIMU WAPEWA NASAHA

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Mahafali ya Shule ya Awali na Msingi Kom ya kuwaaga wahitimu wa darasa la saba na chekechea yamefana, huku wahitimu la Saba wakisisitizwa kuepukana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii, dawa za kulevya na kutojiingiza katika makundi mabaya, bali waendelee kudumisha nidhamu waliyojengewa shuleni hapo.

TAZAMA VIDEO👇👇


Mahafali hayo yamefanyika leo Septemba 19, 2026, huku mgeni rasmi akiwa Afisa Mthibiti Ubora wa Shule katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Edith Mwijage, ambaye pia ni Mratibu wa Idara ya Uthibiti Ubora wa Shule Mkoa wa Shinyanga.
Amesema, anawapongeza wahitimu hao kuonyesha nidhamu ya hali ya juu, na kuwataka wanaporejea majumbani kwao wawe wanafunzi wazuri, huku wakijiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na dawa za kulevya, kwa sababu wanakwenda kukutana na jamii yenye mambo mengi mitaani.

“Wanafunzi ambao mmehitimu darasa la saba, nendeni mkaitangaze Kom kwa kuendelea kuwa na nidhamu nzuri,” amesema Mwijage.
Aidha, ameipongeza shule hiyo kwa kuendelea kufanya vizuri kwa kufaulisha wanafunzi wake kwa daraja la A.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Bodi ya Shule ya Awali na Msingi Kom Beatrice Mark, amewataka wahitimu kuendelea kumtanguliza Mungu kwa kila jambo, pamoja na kuendelea kujitambua na kusimamia ndoto zao.
Aidha, amewataka wazazi kuendelea kuwasimamia watoto wao waliohitimu elimu ya darasa la saba, akisema dunia ya sasa imeharibika, na kumekuwapo na unyanyasaji mkubwa wa kijinsia, pamoja na kuwafundisha namna ya kujilinda dhidi ya unyanyasaji huo.

Mkurugenzi wa Shule za Kom Jackton Koyi, amewashukuru wazazi kwa kuwapeleka watoto wao kusoma katika shule hiyo, akisema waendelee kuwaamini na kwamba hawatawaangusha, bali wataendelea kutoa huduma bora za elimu na kufanya vizuri kitaaluma.

Aidha, amewasihi wahitimu kuendelea kuwa na nidhamu nzuri na upendo wanapokuwa majumbani mwao.
Katika hatua nyingine, amesema Septemba 22, 2026 siku ya Jumanne, kutakuwa na mtihani wa kujiunga na Kidato cha Kwanza katika Shule ya Sekondari Kom, huku fomu ya kujiunga ikigharimu Sh20,000 kwa kila mwanafunzi.

Amesema kwa wanafunzi 83 ambao wamehitimu shule ya Awali na Msingi Kom wenye tayari fomu zao zimeshalipiwa.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi Kom Pius Saye, akisoma taarifa ya shule, amesema tangu kuanzishwa kwa shule hiyo, imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma kwa kupata ufaulu wa daraja A na B.

Kwa upande wa risala ya wanafunzi iliyosomwa na mhitimu, Safina Nobert, amesema walianza shule wakiwa wanafunzi 56, lakini kutokana na mazingira bora na ufaulu mzuri wa shule hiyo, waliongeza wanafunzi wengine na kufikia 83 ambao ndiyo wamehitimu leo.

TAZAMA PICHA 👇👇
Afisa Mthibiti Ubora wa Shule katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Edith Mwijage akizungumza.
Mkurugenzi wa Shule za Kom Jackton Koyi akizungumza.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi Kom Pius Saye akisoma taarifa ya shule.
Wahitimu wakisoma Risala ya Shule.
Mkurugenzi wa Shule za Kom Jackton Koyi akimkabidhi zawadi Mgeni rasmi.
Mgeni Rasmi akikabidhi vyeti kwa wahitimu.


TAZAMA VIDEO👇👇


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464