` KIKUNDI CHAPANG’OMBE CHAZINDULIWA RASMI OLD SHINYANGA, CHAGUSA WATU WENYE UHITAJI

WANDAMAN HOTEL

KIKUNDI CHAPANG’OMBE CHAZINDULIWA RASMI OLD SHINYANGA, CHAGUSA WATU WENYE UHITAJI

 


KIKUNDI CHAPANG’OMBE CHAZINDULIWA RASMI OLD SHINYANGA, CHAGUSA WATU WENYE UHITAJI

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Kikundi cha Chapang’ombe kilichopo OldShinyanga, kimezinduliwa rasmi, huku kikigusa hali za watu wenye uhitaji kwa kuwapatia msaada wa chakula na sabuni.

TAZAMA VIDEO👇👇


Kikundi hicho kimezinduliwa rasmi leo Septemba 12, 2026, na Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Kata ya Kambarage Mariamu Rumakil.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kikundi hicho, Mariamu amekipongeza kwa kuwasaidia watu wenye uhitaji, akisema jambo hilo walilolifanya ni kujipatia thawabu mbinguni.

“Nawapongeza sana kwa kuguswa na watu hawa wenye uhitaji, mtafika mbali na kikundi chenu,” amesema Mariamu.
Pia, amewataka wanakikundi hao kuongeza juhudi kuwa na mshikamano, upendo, kudumisha umoja na amani, akisema hizo ndiyo nguzo zitakazofanya kikundi chao kuwa imara na kuendelea kudumu.

Aidha, amewataka pia kuwa mabalozi wazuri wa kupinga vitendo vya ukatili ndani ya jamii, ili wananchi waishi kwa usalama, amani na upendo.
Naye Mwenyekiti wa kikundi hicho Juma Bugoye, amesema kikundi chao kilianza mwaka 2025, kikiwa na wanachama 12, lakini sasa kimefikia wanachama 100 na leo kimezinduliwa rasmi.

Amesema, shughuli za kikundi hicho ni kusaidiana wakati wa shida na raha miongoni mwa wanachama, pamoja na kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Aidha, amesema mikakati yao ni kuendelea kukijenga zaidi kikundi hicho, pamoja na kuanzisha miradi mbalimbali ambayo itakuwa chanzo cha mapato, huku wakitarajia pia kujenga ofisi yao.

Nao baadhi ya watu wenye uhitaji waliopewa msaada, akiwamo Saraha Mashenene, wamewashukuru wanakikundi hao kwa msaada wa chakula na sabuni, na kuwaomba waendelee kuguswa na kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu.

TAZAMA PICHA👇👇

Mwenyekiti wa UWT Kambarage Mariamu Rumakil akizungumza.
Mwenyekiti wa UWT Kambarage Mariamu Rumakil akizungumza.
Mwenyekiti wa Kikundi cha Chapang'ombe Juma Bugoye akizungumza.
Mwenyekiti wa UWT Kambarage Mariamu Rumakil akikata utepe kuzindua rasmi kikundi cha Chapang'ombe Kata ya Oldshinyanga.
Mwenyekiti wa UWT Kambarage Mariamu Rumakil akikata utepe kuzindua rasmi kikundi cha Chapang'ombe Kata ya Oldshinyanga.
Mwenyekiti wa UWT Kambarage Mariamu Rumakil akikata Keki kuzindua rasmi kikundi cha Chapang'ombe Kata ya Oldshinyanga.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464