Mbunge wa Jimbo la Tabora Mjini, Hawa Mwaifunga, ameanza ziara ya kukagua maeneo mbalimbali yenye changamoto katika Kata ya Chemchem, akiwa ameambatana na Diwani wa kata hiyo, Salum Bandora, kwa lengo la kubaini changamoto na kuweka mikakati ya kuzitatua kwa wakati.
Ziara hiyo imefanyika kufuatia kikao cha kimkakati kilicholenga kutathmini maeneo yenye changamoto, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño.
Katika kikao hicho, Mwaifunga na Bandora walibainisha maeneo yanayohitaji hatua za haraka, ikiwemo mitaro iliyozibwa na mchanga pamoja na taka, uchakavu wa baadhi ya mitaro, maeneo yenye mwelekeo usio sahihi wa mtiririko wa maji na udhaifu wa kingo za Mto Kenge.
Changamoto nyingine zilizobainishwa ni vizuizi vinavyosababishwa na baadhi ya majengo, uwepo wa magari mabovu katika maeneo yanayoweza kuzuia mtiririko wa maji, pamoja na uhitaji wa makaravati katika maeneo mbalimbali ili kurahisisha upitishaji wa maji ya mvua.
Baada ya kubaini changamoto hizo, viongozi hao wamekubaliana kushirikiana na Serikali kuhakikisha maeneo yote yaliyoainishwa yanafikiwa na hatua stahiki zinachukuliwa kwa wakati, hususan katika kipindi hiki cha maandalizi ya msimu wa mvua.
Hatua hiyo imezingatia umuhimu wa kuchukua tahadhari mapema, kwa kuamini kwamba “kinga ni bora kuliko tiba,” huku viongozi hao wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, viongozi wa kata na wananchi katika kuhakikisha usalama wa jamii.
Aidha, Mwaifunga na Bandora wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo, kwa kuzingatia maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu maandalizi na hatua za kukabiliana na athari za majanga.
na hatua stahiki zinachukuliwa kwa wakati, kwa kuzingatia umuhimu wa maandalizi ya mapema katika kuzuia athari za mvua.
Hatua hiyo inaendana na kauli ya “kinga ni bora kuliko tiba,” huku viongozi hao wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya Serikali, viongozi wa kata na wananchi katika kuhakikisha usalama wa jamii wakati wa msimu wa mvua.
Aidha wameahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo, kwa kuzingatia maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu maandalizi na hatua za kukabiliana na athari za majanga.
