Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Wanawake wametakiwa kuchamkia fursa mbalimbali ambazo zinatolewa na serikali, kupitia majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ikiwamo mikopo, ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuendesha familia zao.
TAZAMA VIDEO👇👇
Hayo yamebainishwa leo Septemba 15, 2026 na Mbunge wa Viti Maalumu kundi la vyuo na vyuo vikuu, Dk. Rejina Malima, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Shinyanga, wakati akikabidhi ahadi ya Sh. milioni moja kwa Jukwaa la Wanawake wilayani Kishapu.
Amesema majukwaa ya wanawake yana fursa nyingi za uwezeshaji kiuchumi, hivyo kuwataka wanawake wasibweteke, bali wachangamkie fursa zilizopo, ikiwamo mikopo, ili waweze kuanzisha miradi na kupata vipato.
“Mwezeshaji wa Majukwaa ya Uwezashaji wanawake kiuchumi muasisi wake ni Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye kipindi hicho alikuwa Makamu wa Rais, Majukwaa hayo yana umuhimu sana katika Taifa letu kwa kusaidia wanawake,” amesema Dk. Malima.
Aidha, amempongeza pia Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita kwa kuendelea kusimamia majukwaa hayo na hata kufanya vizuri.
Naye Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi wilayani Kishapu Pendo Msomi, amemshukuru Mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake, akisema fedha hizo wataziongeza na nyingine, ili kuanzisha miradi ya kuwawezesha kujikwamua kiuchumi.
TAZAMA PICHA👇👇
Dk. Regina Malima (kushoto) akikabidhi Sh. Milioni Moja kwa Mwenyekiti wa Jukwaa wa uwezeshaji wanawake kiuchumi wilaya ya Kishapu Pendo Msomi.
Dk. Regina Malima (kushoto) akikabidhi Sh. Milioni Moja kwa Mwenyekiti wa Jukwaa wa uwezeshaji wanawake kiuchumi wilaya ya Kishapu Pendo Msomi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464