Safari rasmi ya championship league 2026/2027 imeanza vizuri kwa *Rhino Rangers* kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo uliopigwa katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, Tabora.
Makamu mwenyekiti wa Rhino Rangers Bandora Salum Mirambo amewapongeza wachezaji kwa kufanya vizuri katika mchezo huo kwani umekua mwanzo mzuri wa kuianza safari ya kuelekea ligi kuu kwa ushindi.
Bandora amewapongeza wana faru wote kwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mechi hiyo akisema uwepo wao ndio siri ya mafanikio katika mchezo huo.
Aidha amewataka mashabiki, wadau na wananchi kuendelea kuishabikia Rhino Rangers na kuiunga mkono ili iweze kufanya vizuri zaidi.
RHINO RANGERS" tumeanza safari ya kurejea ligi kuu kwa ushindi, kituo kinachofuata ni Songea".
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464