FIKRA MPYA WATAMBULISHA MRADI MPYA WA KUSAIDIA MANUSURA WA UKATILI WA KIJINSIA KUPATA HAKI ZAO
Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Shirika la Fikra Mpya, limetambulisha rasmi mradi mpya wa kuwezesha upatikanaji wa haki kwa manusura wa ukatili wa kijinsia (Justice For Survivors J4S) mkoani Shinyanga, ambao utatekelezwa Manispaa ya Shinyanga Kishapu.
TAZAMA VIDEO👇👇
Mradi huo umetambulishwa leo Agosti 17, 2026, na kushirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka serikalini, wakiwamo maafisa ustawi wa jamii, maafisa maendeleo ya jamii, dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi pamoja na watoa huduma za msaada wa kisheria.
Akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo, Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah, amesema mradi huo unalenga kuhakikisha manusura wa ukatili wa kijinsia wanapata haki zao kisheria, kwa lengo la kukomesha vitendo hivyo ndani ya jamii.
“Mradi huu utatekelezwa katika kata nne, ambazo ni Ndembezi na Ngokolo katika Manispaa ya Shinyanga, pamoja na Mwataga na Igaga wilayani Kishapu, maeneo ambayo yana matukio mengi ya ukatili wa kijinsia,” amesema Leah.
Naye Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo, amesema wameupokea mradi huo unaoitwa “Wezesha Upatikanaji wa Haki za Manusura wa Ukatili wa Kijinsia”.
Amesema, mradi huo utatoa huduma kwa manusura wa ukatili wa kijinsia, hasa katika kuwawezesha kupata haki zao kisheria.
Amesema, mradi huo umewaleta pamoja wadau mbalimbali, ili kuona namna bora ya kuwasaidia manusura wa ukatili wa kijinsia kupata huduma za kisheria na kiafya.
TAZAMA PICHA👇👇
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah akizungumza.
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah akizungumza.
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah akizungumza.
Mkurugenzi wa Shirika la Fikra Mpya Leah Josiah akizungumza.
Afisa Ustawii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo akizungumza.
Afisa Ustawii Mkoa wa Shinyanga Lidya Kwesigabo akizungumza.