` KIMBUNGA CHA MAENDELEO YA MBUNGE AZZA JIMBO LA ITWANGI CHAMG’OA KIGOGO CHADEMA, ZIARA YA KIJIJI KWA KIJIJI

WANDAMAN HOTEL

KIMBUNGA CHA MAENDELEO YA MBUNGE AZZA JIMBO LA ITWANGI CHAMG’OA KIGOGO CHADEMA, ZIARA YA KIJIJI KWA KIJIJI

 

KIMBUNGA CHA MAENDELEO YA MBUNGE AZZA JIMBO LA ITWANGI CHAMG’OA KIGOGO WA CHADEMA ZIARA YA KIJIJI KWA KIJIJI

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad amendelea na ziara yake ya kijiji kwa kijiji awamu ya pili kwa kusikiliza kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi, huku akielezea miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ameifanya kwa kipindi chake kifupi cha ubunge.

TAZAMA VIDEO👇👇


Kutokana na kuelezea utekelezaji wa miradi hiyo ya maendeleo ambayo inaonekana kwa vitendo chini ya utawala wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, Kada wa CHADEMA Jackson Kulwa kujiunga CCM ili kuunga mkono Juhudi za maendeleo.
Azza akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ishololo Kata ya Usule Jimbo la Itwangi, amesema changamoto ya kwanza ambayo anaijua katika kijiji hicho ni Maji, na kwamba kutokana na kulijua tatizo hilo na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, alisema kwamba badala ya kusubili wananchi wapate maji ya Ziwa Victoria, ni vyema wakachimbiwa kwanza kisima kirefu ili wapate maji.

Amesema, licha ya kuwapo kwa maji hayo lakini vituo vya kuchotea maji ni kimoja na kueleza kwamba atazungumza na watu wa RUWASA ili kuongeza vituo vingine viwili.
Aidha, amesema licha ya wananchi kuendelea kutumia maji ya kisima kirefu, hakukaa kimya bali aliendelea kuzungumzia upatikanaji wa Maji ya Ziwa Victoria na ,kwama Serikali imeshatuma wataalaamu wake na upembuzi yakinifu umeshafanyika kwa Kata nzima ya Usule ili kuanza utekelezaji wa mradi huo.

“Mradi huu wa maji ya Ziwa Victoria kufika Kata ya Usule utatumia Tangi la Maji la Imesela,”amesema Azza.
Amezungumzia pia utatuzi wa kero ya barabara ya muda mrefu kutoka Usule kwenda Tinde, kwamba alikwenda kuisemea na serikali chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ikatoa fedha za dharura na kujengwa.

Aidha, amezungumzia bwawa la maji la Ishololo, kwamba licha ya kukwama ujenzi wake nalo ameshalisemea bungeni ili likamilike na kujengwa.
Amesema katika suala ya huduma ya umeme, kwamba Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM inasema kuanzia 2025 hadi 2030 vitongiji vyote vitakuwa na umeme na kwamba katika Jimbo hilo la Itwangi katika awamu hii ya usambazaji umeme ngazi ya vitongoji wamepata vitongoji 58, na hivyo kuwataka wananchi wawe na subira sababu wote watapata umeme.

“Nawaomba wenyeviti wa vitongoji, muda utakapofika wa kuletewa umeme wa REA toeni ushirikiano wa kutosha kwa watu wa REA ili wananchi wapate huduma hiyo,” amesema Azza.
Amezungumzia pia utatuzi wa changamoto ya daraja la kutoka Kijiji cha Ishololo kwenda Igalamya kwamba suala hilo analichukua na atakwenda kulifanya kazi, huku akiwasihi wananchi hao kuanzisha pia ujenzi wa Zahanati na kuifikisha hatua ya Renta ili aone namna ya kuwaunga mkono na serikali kuikamilisha na kutoa huduma.

Kwa upande wake Meneja Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) wilaya ya Shinyanga Mhandisi Emmael Nkopi, amesema suala la kuongeza vituo hivyo vya kuchotea maji, kwamba atapeleka wataalamu wake kuangalia namna ya kuongeza vituo hivyo viwili huku akibainisha kuwa mradi wa maji ya Ziwa Victoria katika Kata hiyo ya Usule utekelezaji wake utaanza mwakani.
Aidha, aliyekuwa Katibu Kata wa CHADEMA Kata ya Usule zaidia ya miaka 15 Jackson Kulwa, amesema kutokana na kasi ya maendeleo wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, ameamua kuchukua uamuzi wa kurudisha Kadi ya CHADEMA na kujiunga na CCM.

Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad ameendelea na ziara ya kijiji kwa kijiji awamu ya pili kwa kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia majibu pamoja na kuelezea utekelezaji wa miradi ya maendeleo chini ya Utawala wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.

TAZAMA PICHA NA ELIZABETH COSMAS 👇👇

Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ishololo.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ishololo.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akisikiliza kero za wananchi wa Ishololo.

TAZAMA VIDEO👇👇
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464