Balozi wa King D Pikipiki, Barnaba Classic akitumbuiza wakati wa uzinduzi rasmi wa pikipiki mpya za King D uliofanyika mjini Shinyanga, Septemba 21, 2026.

Mkurugenzi wa King D, Dustan Philbert, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa pikipiki mpya za King D uliofanyika mjini Shinyanga, Septemba 21, 2026.

Balozi wa Nyorobi Pikipiki na Spea Hussein Abdullah, maarufu Manoma Action akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa pikipiki mpya za King D uliofanyika mjini Shinyanga, Septemba 21, 2026.
Na Mwandishi Wetu, Malunde 1 blog
Kampuni ya King D Pikipiki imezindua rasmi pikipiki zake mpya katika soko la Mkoa wa Shinyanga, huku Nyorobi Pikipiki na Spea ikitangazwa kuwa msambazaji na muuzaji rasmi wa pikipiki hizo pamoja na spea zake halisi kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Uzinduzi huo umefanyika leo, Septemba 21, 2026, mjini Shinyanga, katika hafla iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali, wafanyabiashara na wapenzi wa pikipiki, pamoja na msanii maarufu wa Bongo Fleva, Elias Barnabas Inyasi, anayefahamika zaidi kwa jina la Barnaba Classic, ambaye ni Balozi Mkuu wa King D Pikipiki.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa King D, Dustan Philbert, amesema kampuni hiyo imekuja na pikipiki zilizolenga kukidhi mahitaji ya watumiaji kwa kuzingatia ubora, teknolojia ya kisasa, ufanisi na usalama wa mtumiaji.
Dustan amewashukuru wateja na wadau mbalimbali kwa mapokezi mazuri waliyoyatoa kwa King D, akieleza kuwa pikipiki hizo zimeundwa kwa kutumia vifaa na teknolojia inayolenga kumpatia mtumiaji uzoefu bora wakati wa matumizi.
“Nawashukuru sana kwa mapokezi yenu mazuri. Niwaambie kuwa pikipiki hizi zimetengenezwa kwa ubora, ikiwemo vifaa vya kisasa vyenye uwezo mkubwa,” amesema Dustan.
BARNABA: KING D IMEKAGULIWA KWA UMAKINI
Kwa upande wake, Balozi wa King D Pikipiki, Barnaba Classic, amesema amekuwa sehemu ya mchakato wa kujiridhisha kuhusu ubora wa pikipiki hizo kabla ya kuanza kuzitangaza kwa watumiaji.
Amesema King D imezingatia ubora wa pikipiki pamoja na upatikanaji wa spea zake, huku akieleza kuwa bei na ubora wake vinalenga kuwapa watumiaji chaguo linaloweza kukidhi mahitaji yao.
Barnaba Classic
“Tumejiridhisha kwa kukagua kifaa kimoja hadi kingine, maana tulijua mnapenda vitu vizuri. King D Pikipiki na spea zake zinapatikana kwa bei nafuu, na utakapoimiliki utagundua kuna utofauti na pikipiki nyingine,” amesema Barnaba.
NYOROBI YAHAKIKISHA UPATIKANAJI WA KING D KANDA YA ZIWA
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Nyorobi Pikipiki na Spea bwana Michael Nyorobi , Balozi wa Nyorobi Pikipiki na Spea Hussein Abdullah, maarufu Manoma Action, amesema Nyorobi imejipanga kuhakikisha wateja wanapata pikipiki za King D pamoja na spea zake halisi kwa urahisi.
Ameeleza kuwa wateja wanaohitaji pikipiki hizo wanaweza kufika Nyorobi Pikipiki na Spea kwa ajili ya kupata huduma na maelezo zaidi kuhusu bidhaa hizo.
“Tunawashukuru wateja wote wa Nyorobi. Hakikisha haukosi pikipiki hizi, maana zinapatikana kwa wingi na zimetengenezwa na Mtanzania mwenzetu. Tumuunge mkono, maana King D ni Mfalme wa Barabarani,” amesema Manoma.
KING D YAFUNGUA SOKO JIPYA SHINYANGA
Uzinduzi huo unaifanya King D Pikipiki kuingia rasmi katika soko la Shinyanga na Kanda ya Ziwa, huku Nyorobi Pikipiki na Spea ikiwa sehemu muhimu katika kuhakikisha pikipiki hizo na spea zake zinawafikia watumiaji.
Kwa wafanyabiashara, waendesha bodaboda na watumiaji wengine wanaohitaji pikipiki, uzinduzi huo unatoa fursa ya kuifahamu King D, kuiona pikipiki hiyo kwa karibu na kupata taarifa kuhusu upatikanaji wa pikipiki pamoja na spea zake halisi.
KING D – MFALME WA BARABARANI.
Mkurugenzi wa Nyorobi Pikipiki na Spea ,Michael Nyorobi (kulia) na Balozi wa King D Pikipiki, Barnaba Classic wakikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa pikipiki mpya za King D uliofanyika mjini Shinyanga, Septemba 21, 2026.
Uzinduzi wa pikipiki mpya za King D ukifanyika mjini Shinyanga, Septemba 21, 2026.
Mkurugenzi wa King D, Dustan Philbert, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa pikipiki mpya za King D uliofanyika mjini Shinyanga, Septemba 21, 2026.
Mkurugenzi wa King D, Dustan Philbert, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa pikipiki mpya za King D uliofanyika mjini Shinyanga, Septemba 21, 2026.
Balozi wa King D Pikipiki, Barnaba Classic akitumbuiza wakati wa uzinduzi rasmi wa pikipiki mpya za King D uliofanyika mjini Shinyanga, Septemba 21, 2026.
Balozi wa King D Pikipiki, Barnaba Classic akitumbuiza wakati wa uzinduzi rasmi wa pikipiki mpya za King D uliofanyika mjini Shinyanga, Septemba 21, 2026.
Balozi wa King D Pikipiki, Barnaba Classic akitumbuiza wakati wa uzinduzi rasmi wa pikipiki mpya za King D uliofanyika mjini Shinyanga, Septemba 21, 2026.
Balozi wa King D Pikipiki, Barnaba Classic akiwa na Balozi wa Nyorobi Pikipiki na Spea Hussein Abdullah, maarufu Manoma Action wakati wa uzinduzi rasmi wa pikipiki mpya za King D uliofanyika mjini Shinyanga, Septemba 21, 2026.
Balozi wa Nyorobi Pikipiki na Spea Hussein Abdullah, maarufu Manoma Action akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa pikipiki mpya za King D uliofanyika mjini Shinyanga, Septemba 21, 2026.

Muonekano wa sehemu ya pikipiki za King D
Balozi wa King D Pikipiki, Barnaba Classic na Mkurugenzi wa Nyorobi Pikipiki na Spea ,Michael Nyorobi (kulia).

Mkurugenzi wa Nyorobi Pikipiki na Spea ,Michael Nyorobi akiwa na Balozi wa King D Pikipiki, Barnaba Classic na Mkurugenzi wa King D, Dustan Philbert (katikati)