` KITIMA ATIKISA MISINGI YA BIBLIA YA MAMLAKA NA UCHUMI

KITIMA ATIKISA MISINGI YA BIBLIA YA MAMLAKA NA UCHUMI



Uchambuzi wa kauli ya Padri Charles Kitima unaonesha kuwa, mbali na mgawanyiko wa kijamii, kiongozi huyo anaonekana kukiuka misingi mikuu ya Biblia na kuhatarisha uchumi wa nchi. Kauli za siasa zenye uhasama siku zote hutishia kuvunja amani ambayo ndio msingi mkuu wa maendeleo.

Kiuchumi, nchi inahitaji utulivu ili kuvutia wawekezaji. Kauli zinazoonesha kutokuwepo kwa utulivu au kuashiria vurugu, huwafanya wawekezaji kupoteza imani. Kama ilivyosisitizwa: "Pasina AMANI hamna maendeleo." Hivyo basi, kauli hizi zinatafsiriwa kama "kunufaisha maadui wa nchi kuliko wananchi" kwani zinakwaza juhudi za kujenga uchumi.

Ki-Bibilia, wachambuzi wamekerwa na namna ambavyo Padri Kitima ameacha wajibu wake wa kiroho wa kuwa mpatanishi. Biblia inasisitiza utii kwa mamlaka iliyopo (Warumi 13:1), na kuonesha hekima na busara katika ushauri, badala ya uchochezi. "Wakati Yesu alitambua uongozi kwa kuwaambia wafuasi wake wampe Kaizari ya kwake na Mungu yake na kutambua uhakimu wa Herode, swali linalowekwa mbele ya umma ni ulinganifu wa kauli za Padri Kitima na Maandiko Matakatifu.

Wakati Rais ananyoosha mkono akisema "yaliyopita si ndwele" na akisihi "tugange yajayo", Padri Kitima amechagua kudandia na kushadidia yaliyopita. Matendo haya yanaonesha yeye "ana shauku ya kuendelea kuona mambo mabaya yakitokea," akitumia vibaya ushawishi wake kuaminisha waumini kuwa Serikali ni katili.

Hatimaye, ni muhimu kukumbuka busara ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliyesema: "Kosa moja kubwa sana ambalo pia linatokana na ubinafsi ni kutaja makosa ambayo sisi wenyewe hatunayo, na kuficha makosa ambayo sisi wenyewe tunayo." Kauli hii inawafaa viongozi kama akina Padri Kitima kujitathmini.Kwa kujitathmini pekee tunaweza kujihoji kama "Fr. Kitima anajituma, anatumwa au anatumika?". Na katika hilo ni lazima kupata jibu ili isibaki kuwa fumbo.

 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464