Na Marco Maduhu, SHINYANGA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, ameongoza zoezi la utoaji tuzo kwa shule zilizofanya vizuri kitaaluma mkoani humo 2025, huku akizitaka shule zilizofanya vibaya kuongeza juhudi na ubunifu ili kuinua viwango vya ufaulu.
Hafla hiyo imefanyika leo Februari 23, 2026, kwenye kikao cha wadau cha tathmini ya utekelezaji wa shughuli za elimu mkoani Shinyanga, kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya Sekondari ya wasichana Shinyanga.
Mhita, akizungumza kwenye hafla hiyo, amezipongeza shule ambao zimefanya vizuri kitaaluma, na kuzitaka zile ambazo zimefanya vibaya ziongeze juhudi na ubunifu katika kufundisha wanafunzi, ili nazo zifanye vizuri kitaaluma.
“Nazipongeza shule zote ambazo zimepata Tuzo kwa kufanya vizuri kitaaluma, na zile ambazo zimefanya vibaya ziongeze juhudi ili katika utoaji wa Tuzo hizi tena, kusiwepo na shule hata moja, itakayopewa ya kufanya vibaya,” amesema Mboni.
Ametoa pia maagizo, kufuatilia zoezi la uandikishaji wanafunzi kuanza shule kwa wale wote ambao wamefikisha umri wa kuanza masomo, na wale waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, wahudhurie masomo, kuhamasisha uchangiaji wa chakula shuleni, ili wanafunzi wapate kula na kuzingatia masomo.
Maagizo mengine ni kusimamia miradi ya elimu na ikamilike kwa wakati, usimamizi wa taaluma na maendeleo ya shule pamoja na kuingia mikataba kati ya wakuu wa shule na walimu, kusikiliza kero za walimu na kuzitatua, walimu kutulia kwenye vituo vya kazi, kudhibiti utoro pamoja na mdondoko wa wanafunzi.
Aidha, amewasihi wazazi kupeleka watoto wao shule, wakiwamo na wenye ulemavu na kwamba elimu ni bure na haina haja kuwanyima fursa ya kupata elimu, sababu pia ni kosa kisheria.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Samson Hangwa, akisoma taarifa ya hali ya elimu, amesema kiwango cha ufaulu kimeongezeka mkoani humo ikilinganishwa na mwaka jana.
Baadhi ya wakuu wa shule zilizopata tuzo wamesema mafanikio yao yametokana na utoaji wa chakula shuleni, ushirikiano mzuri kati ya wazazi na walimu, kufanya mitihani ya mara kwa mara, kudhibiti utoro na kutoa motisha kwa walimu.
TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza kwenye hafla hiyo ya kutunuku Tuzo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akizungumza.
Mkuu wa wilaya Kahama Frank Nkinda akizungumza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Samson Hangwa akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza.
Muonekano wa Tuzo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akitoa Tuzo kwa shule ambazo zimefanya vibaya.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akitunuku Tuzo kwa shule ambazo zimefanya vizuri kitaaluma.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464