Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wamemchagua Diwani wa Kata ya Imesela Seth Anthony Msangwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, akichukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ngassa Mboje.
Uchaguzi huo umefanyika leo Desemba 2,2025 mara baada ya madiwani kumaliza kuapishwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Nido Olivia Bisaga.
Awali msimamizi wa Uchaguzi huo Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Said Kitinga, amesema idadi ya wapiga kura walioandikishwa ni 38, lakini wajumbe waliopiga kura ni 36, na kati ya kura hizo Seth Anthony Msangawa amepata kura zote 36.
Amemtangaza pia Joseph John Buyugu kuwa ndiye ameshinda nafasi ya Umakamu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kupata na yeye kura 36.
"kwa Mamlaka niliyonayo na mtangaza Seth Anthony Msangwa ndiye Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, pamoja na Joseph John Buyugu kuwa ndiye Makamu Mwenyekiti,"ametamka Kitinga.
Naye Mwenyekiti huyo Mpya bwana Seth, ameshukuru Madiwani hao kwa kumchagua, huku akiomba ushirikiano na kufanya kazi kama "Teamwork".
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dk.Kalekwa Kasanga, ameahidi madiwani ushirikiano wa kutosha kwa ajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo la Halmashauri hiyo.
Aidha,baada ya kutangaza matokeo hayo, ziliundwa pia Kamati Mbalimbali za kudumu za Halmashauri hiyo.
TAZAMA PICHA👇👇
Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Seth Anthony Msangwa akizungumza.
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Joseph Buyugu akizungumza.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk.Kalekwa Kasanga akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akizungumza.
Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Seth Anthony Msangwa (kulia)akiwa na Makamu wake Joseph John Buyugu.
Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad (kushoto)akiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela.
Madiwani wakila kiapo.
Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad akipiga kura kuchagua Mwenyekiti na Makamu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Picha za pamoja zikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464