Kutokana na ukweli huo vurugu siyo jawabu. Vurugu hufunga milango, huharibu miradi, na inatishia amani ambayo inatuletea fursa zote hizi. Tunapoona watoto, wazee, vilema, na wanawake ambao hawawezi kuishi kwenye vurugu, tunakumbushwa umuhimu wa amani yenye haki ili kurudisha nchi yetu kwenye hadhi yake ya Kisiwa cha Amani Duniani.
Katika mazingira ya kisasa zaidi wenye uwezo wa kubadilisha Taifa ni vijana na uwezo huo upo mikononi mwao. Ili kuleta mafanikio hayo ni dhahiri vijana wanatakiwa kuanzia leo kuwa balozi wa amani nyumbani kwake, mwambie mwenzako naye amwambie mwenzake. Amani na haki ndiyo njia pekee ya kufanya maisha ya Watanzania yawe ya furaha.
Serikali imetambua uwezo wetu kama wana-mapinduzi katika sekta zote za uchumi. Hatua madhubuti zimechukuliwa kuimarisha ushiriki wetu katika kuinua uchumi ni pamoja na kuanzishwa kwa Wizara kamili ya Vijana chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Joel Nanauka na uwepo wa ahadi ya kutoa shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kuongeza mitaji kwa shughuli za kiuchumi za Vijana na Wanawake.
Kama alivyosema Mhe. Nanauka: "Vijana Kila Kona fursa zimetanda, kazi yetu ni kuzisaka na kuzipata ili tuwe chanzo Cha ukuaji wa uchumi wetu."
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464