Na Marco Maduhu,DODOMA
MSEMAJI wa Jeshi la Polisi Tanzania DCP David Misime, amewataka waandishi wa habari na vyombo vya habari kwa ujumla kuepuka kuchapisha taarifa zinazoweza kuchochea chuki na kuhatarisha usalama wa nchi.
Hayo yamebainishwa leo Novemba 27,2025 kwenye mafunzo ya uandishi wa habari za amani Jijini Dodoma yaliyoandaliwa na Taasisi ya vyombo vya habari Kusini Mwa Afrika Tawi la Tanzania MISA-TAN.
Amesema vyombo vya habari hasa vya mitandaoni wamekuwa wakiandika habari kwa mlengo wa kupata fuasi (views)bila hata ya kuchuja habari na kuiangalia ima madhara gani kwa taifa na kuipeleka hewani tu, na hatimaye kuhatarisha usalama wanchi.
“Katika habari hizi za amani,nawaomba waandishi muepuke kutoa habari zinazojenga chuki na kuhatarisha usalama wa nchi, na pia mtoe taarifa sahihi zenye kujenga na siyo kubomoa zilizo thibitishwa na mamlaka husika na zisizoengemea upande mmoja,”amesema DCP Misime.
Ameongeza pia kuepuka kuandika habari za upotoshaji na lugha za chuki hata kama habari hizo zinatoka kwenye matamko ya siasa, bali wasizipe nafasi habari hizo ili kulinda amani ya nchi.
Aidha,amesisitiza kuwa waandishi wa habari waendelee kutoa taarifa zinazohamasisha uzalendo,umoja,mshikamano na amani hasa katika kipindi hiki.
“Hizi taarifa za kuhamasisha amani,uzalendo na Mshikamano ndipo kipindi ambacho wanapaswa kulivalia njuga.”amesema DCP Misime.
Awali Mwenyekiti wa MISA TANZANIA Edwin Soko, amesema wameletwa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuandika habari za kuhamasisha amani, kupunguza taarifa za uchochezi, upotoshaji, kuchambua habari za kuchochea migogoro, na kuandika habari za kuhamasisha umoja amani na mshikamano wa taifa.
TAZAMA PICHA👇👇
Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania DCP David Misime akizungumza.
Mwenyekiti wa MISA TANZANIA Edwin Soko akizungumza.
Mwenyekiti wa MISA TANZANIA Edwin Soko akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464