Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MJUMBE wa Kamati ya siasa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)wilaya ya Shinyanga Mjini Mhandisi James Jumbe, alishiriki kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025.
Alipiga kura katika kituo kilichopo Miti Mirefu Mtaa wa Majengo Kata ya Kambarage.
Oktoba 29,2025 ilikuwa ni siku ya Uchaguzi Mkuu kwa wananchi kupiga kura na kuwachagua Madiwani,Wabunge na Rais ambao watawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano 2025-2030.
Akizungumza mara baada ya kupiga kura,alisema amejisikia furaha kutimiza takwa la Kikatiba na kuwachagua viongozi anawaotaka kumuongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
“nimejisikia furaha kutimiza takwa la kikatiba kupiga kura na kuwachagua viongozi ninaowataka kuniongoza kwa miaka mitano 2025-2030,”amesema Mhandisi Jumbe.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464







