` KATAMBI ALIVYOPIGA KURA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29

KATAMBI ALIVYOPIGA KURA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MBUNGE Mteule wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Patrobas Katambi,alivyotumia haki yake ya kikatiba kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29,2025.
Katambi alipiga kura katika Kituo cha shule ya Sekondari Chamaguha.

Akizungumza mara baada ya kumaliza kupiga kura,aliwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwao kwa wingi kuwachagua viongozi wanao wataka, na kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu.

“Nimeshiriki kupiga kura na kutumia haki yangu ya kikatiba kuchagua viongozi,”amesema Katambi.

Oktoba 29,2025 ilikuwa ni siku ya Uchaguzi Mkuu kwa wananchi kupiga kura na kuwachagua Madiwani,Wabunge na Rais ambao watawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano 2025-2030.
Amesema, amefarijika kuona wajawazito,wanawake wenye watoto wadogo na watu wenye ulemavu kupewa kipaumbele kupiga kura bila ya kupanga foleni.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464