` DC MTATIRO ALIVYOSHIRIKI KUPIGA KURA OKTOBA 29

DC MTATIRO ALIVYOSHIRIKI KUPIGA KURA OKTOBA 29

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,alishiriki kupiga kura, katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29,2025.

Alipiga kura katika Kituo kilichopo Ukumbi wa Manispaa ya Shinyanga.
Amesema ameshiriki kupiga kura na kutumia haki yake ya kikatiba, kuwachagua viongozi anaowataka.

Oktoba 29,2025 ilikuwa ni siku ya Uchaguzi Mkuu kwa wananchi kupiga kura na kuwachagua Madiwani,Wabunge na Rais ambao watawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano 2025-2030.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464