` KAGUNZE ALIVYOSHIRIKI KUPIGA KURA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 29

KAGUNZE ALIVYOSHIRIKI KUPIGA KURA UCHAGUZI MKUU WA OKTOBA 29

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKURUGENZI wa Manispaa ya Shinyanga Alexius Kagunze,alitumia haki yake ya kikatiba kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 29.

Alipiga kura katika kituo cha ukumbi wa Manispaa ya Shinyanga.
Alisema uchaguzi ulikwenda vizuri, na amepiga kura kuwachagua viongozi anaowataka.

“Uchaguzi umekwenda vizuri, na mimi nimeshiriki kutumia haki yangu ya kikatiba kupiga kura, na kuwachagua viongozi ambao wataniongoza kwa kipindi cha miaka mitano,”amesema Kagunze.

Oktoba 29,2025 ilikuwa ni siku ya Uchaguzi Mkuu kwa wananchi kupiga kura na kuwachagua Madiwani,Wabunge na Rais ambao watawaongoza kwa kipindi cha miaka mitano 2025-2030.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464