` TRA YAIPONGEZA BARRICK KWA ULIPAJI MZURI WA KODI NA UZINGATIAJI WA SHERIA NA KANUNI ZA NCHI

TRA YAIPONGEZA BARRICK KWA ULIPAJI MZURI WA KODI NA UZINGATIAJI WA SHERIA NA KANUNI ZA NCHI

Picha ya pamoja ya ujumbe wa TRA na wafanyakazi wa Barrick
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda akitoa ngao ya mlipa kodi nzuri kwa Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Bw. Leon Ebondo
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda na Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Bw. Leon Ebondo wakibadilishana mawazo.

**
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeipongeza kampuni ya Barrick nchini ambayo inaendesha shughuli zake kwa ubia na serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga kwa kuchangia pato la Taifa kwa kuwa mlipa kodi mzuri sambamba na kufuata sheria za nchi.

Pongezi hizo zimetolewa na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda, baada ya kufanya ziara katika mgodi wa Barrick Bulyanhulu uliopo Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja (Customer Service Week).

Kamishna Mwenda ambaye ameongozana na ujumbe wa maofisa wa mamlaka hiyo amesema wameamua kuwatembelea Mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa sababu unalimikiwa na kampuni kubwa na ni walipa kodi wazuri.

“Migodi ya Barrick Bulyanhulu na Barrick North Mara ni wachimbaji wakubwa wa madini hapa nchini ni walipa kodi wakubwa na wazuri , tumewatembelea ili kujua changamoto zao katika shughuli za uchimbaji wa madini na kuangalia namna ya kuzitatua,” amesema Mwenda.
Amesema migodi ya Barrick licha ya kuwa walipakodi wazuri pia imeajiri idadi kubwa ya wafanyakazi ambao wanalipa kodi sambamba na wakandarasi pamoja na wazabuni wanaofanya nao kazi na kuchangia katika ulipaji wa kodi ambapo wakijengewa mazingira mazuri watachimba madini zaidi na Serikali kukusanya zaidi kodi kutokana na uwekezaji wao.”

Ameongeza kwamba mamlaka ya mapato ni mshirika (Partner) kwa walipa kodi wote hapa nchini hivyo wanatembelea walipa kodi ili kujua changamoto zao za kikodi kujifunza ni kodi zipi zinastahili na zipi hazistahili.

Pia amepongeza mchango mkubwa wa kampuni katika kufanikisha miradi mikubwa ya kijamii.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi wa Barrick Bulyanhulu Bw. Leon Ebondo, amemshukuru Kamishna Mkuu wa TRA na Ujumbe wake kwa kufanya ziara mgodini hapo, na kuwasikiliza kwa lengo la kufanyia kazi na changamoto zao.

Bw. Ebondo amesema mgodi wa Barrick Bulyanhulu umeajiri wafanyakazi wengi wenye ajira za kudumu na wakandarasi wake mbalimbali ambapo pia wapo wananchi wanaotoka katika vijiji vinavyozunguka mgodi wamekuwa wakipata ajira za muda.
Ujumbe wa TRA ukitembelea sehemu mbalimbali za mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Ujumbe wa TRA ukitembelea sehemu mbalimbali za mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Ujumbe wa TRA ukitembelea sehemu mbalimbali za mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Ujumbe wa TRA ukitembelea sehemu mbalimbali za mgodi wa Barrick Bulyanhulu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda akiongea na Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda akiwa kwenye kikao na Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu

Wafanyakazi wa Barrick wakimsikiliza Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Yusuph Juma Mwenda

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464