` UWABABU WAFANYA SHEREHE YA KUTIMIZA MIAKA 10,WACHAGUA VIONGOZI WAPYA

UWABABU WAFANYA SHEREHE YA KUTIMIZA MIAKA 10,WACHAGUA VIONGOZI WAPYA

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

UMOJA wa akina Baba wa Bushushu( UWABABU) katika Manispaa ya Shinyanga,wamefanya sherehe ya kutimiza miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, pamoja na kuchagua viongozi wapya watakao waongoza kwa kipindi cha miaka mitatu.
Sherehe hiyo imefanyika leo Januari 12,2026 iliyotanguliwa na mkutano mkuu wa wanachama, na kumalizika na uchaguzi  wa kuchagua viongozi wapya.

Mgeni Rasmi Afisa Tarafa ya Samuye Aron Laizer akimwakilisha Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Said Kitinga, amepongeza kuanzishwa kwa umoja huo, ambapo utawasaidia katika shughuli zao za kijamii, na kuinuana kiuchumi kupitia kukopeshana.

Amewataka wanachama hao, kuendelea kuwa wamoja, kusimamia miongozo, kanuni na sheria zao, ili waweze kufikia malengo yao.
"nawapongeza sana Umoja wa akina Baba wa Bushushu (UWABABU)kwa kuanzisha umoja wenu kwa ajili ya kusaidiana kwenye shida na raha, na kuinuana kiuchumi kupitia mikopo," amesema Laizer.

Awali, aliyekuwa Katibu wa kikundi hicho Laurent Mabala akisoma taarifa amesema umoja huo ulianzishwa mwaka 2014 na kusajiliwa rasmi 2015,na sasa wapo wanachama 71.
Ametaja malengo ya kikundi hicho kuwa ni kukamilisha ujenzi wa ofisi, kuanzisha SACCOS, miradi ya uzalishaji mali, na kununua kiwanja kujenga ukumbi wa kikundi kwa ajili ya kuongeza mapato.

Aidha, katika uchaguzi huo nafasi ya Mwenyekiti mpya wa kikundi hicho, ameshinda Anorld Makombe na Makamu wake Enyasi Mgambi.

Nafasi ya Katibu mpya wa kikundi hicho ameshinda Elias Bundala, na msaidizi wake Anorld Rweshabula.

Mwenyekiti mpya wa kikundi hicho Anorld Makombe, amewaomba wanachama hao kumpatia ushirikiamo katika kipindi chake cha miaka mitatu ya uongozi wake.

TAZAMA PICHA👇👇
Mgeni Rasmi Afisa Tarafa ya Samuye Aron Laizer akimwakilisha Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akizungumza kwenye sherehe hiyo na mkutano mkuu wa kikundi hicho.
Mwenyekiti mpya wa kikundi cha Uwababu Anorld Makombe akizungumza.
Viongozi wapya wa kikundi cha Uwababu waliochaguliwa.
Mkutano mkuu ukiendelea klabla ya sherehe.
Kikundi cha Uwababu wakila chakula cha pamoja na wenza wao.
Picha za pamoja zikipigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464