Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM Patrobas Katambi,amekutana na akina Mama wa Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga,kuwahamasisha kesho wajitokeze kwa wingi kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais,Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Amekutana nao leo Oktoba 11,2025,ambapo Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kesho Oktoba 11 atakuwa Mjini Shinyanga kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa Kampeni kwa kunadi sera la ilani ya CCM na kuwaelezea mambo ya maendeleo ambayo amefanya kwa miaka mitano iliyopita na atakwenda kufanya nini miaka mingine mitano.
Katambi akizungumza na akina mama hao amewaomba wasikose kwenye mkutano huo wa Kampeni ili kusikiliza sera za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464