` RC MBONI MHITA AFANYA ZIARA SHYDC UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEO

RC MBONI MHITA AFANYA ZIARA SHYDC UKAGUZI MIRADI YA MAENDELEO

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amefanya ziara ya kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, pamoja na kufanya mkutano wa hadhara kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha Bugogo.
Amefanya ziara hiyo leo Januari 7, 2026 akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali wa Serikali na Chama, pamoja na Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad.

Akizungumza kwenye ukaguzi huo wa miradi ya maendeleo, ambapo alikagua ujenzi wa Maabara mbili za Sayansi katika Shule ya Sekondari Igalamya, na ujenzi wa vyumba vitano vya Madarasa, na Matundu 12 ya vyoo katika shule ya Msingi Bugogo, ambapo amepongeza utekelezaji wa miradi hiyo, na kuagiza ikamilike kwa wakati na thamani ya fedha ionekane.

Amesema serikali chini ya Rais. Dk.Samia Suluhu Hassan, imekuwa ikitoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na kwamba wao wasaidizi wake ngazi ya Mkoa wanafanya ziara hizo, ili kuona thamani ya fedha kwenye utekelezaji wa miradi hiyo, na kuisimamia ikamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa.
“Rais Dk.Samia Suluhu Hassan yupo mstari wa mbele kuongoza kwa vitendo kwa kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma zote za kijamii, na ndiyo maana amekuwa akitoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na sisi tunaisimamia miradi hii, ili iwe na ubora na kutoa huduma stahiki,” amesema Mhita.

Ameiagiza pia Halmashauri, wawe wanatenga bajeti za fedha za mapato ya ndani, na kuweka vipaumbele kwenye miradi ya Serikali ili kuikamilisha kwa wakati, na siyo hadi kusubiri fedha kutoka Serikali Kuu, ukiwamo na ukamilishaji wa ujenzi wa Maabara moja katika Secondari ya Igalamya.
Ametoa pia maelekezo kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wilayani humo, kutoa elimu kwa wananchi juu ya kuchangamkia fursa za mikopo ya Halmashauri asilimia 10, na mikopo ya Wajasiriamali ili kuwa kwamua kiuchumi.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa akizunguma kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Bugogo, ametoa Rai kwao kuwapatia fursa ya kusoma watoto wa kike, na siyo kuwabagua na kuwaozesha ndoa za utotoni kwa tamaa ya kupata Ng’ombe , ili nchi iweze kupata watalaamu wake wa baadae.
Aidha, amesema changamoto zote ambazo wameziwasilisha wananchi kwenye mkutano huo, ikiwamo ya ukosefu wa huduma ya umeme, maji na ubovu wa miundombinu ya barabara, kwamba changamoto zote hizo zitatatuliwa.

Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad, akizungumza kwenye mkutano huo, amemshukuru Rais. Dk. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kutoa fedha na kutekelezwa Miradi ya mbalimbali Maendeleo, ukiwamo na uboreshaji wa Shule ya Msingi Bugogo.

Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Dk. Kalekwa Kasanga, akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba Vitano vya Madarasa na Matundu 12 ya vyoo shule ya Msingi Bugogo, amesema Serikali kuu imetoa sh. milioni 157.4 kupitia mradi wa Boost.
Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Igalamya Mathew Mwinuka, akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba viwili vya Maaabara za Sayansi, amesema serikali imetoa sh. milioni 60, na ujenzi upo hatua za ukamilishaji.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita (kushoto)akiwa na Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad, wakipikia mafundi chakula wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita (kushoto)akiwa na Mbunge wa Itwangi Azza Hillal Hamad, wakipikia mafundi chakula wakati wa ziara ya ukaguzi wa utekeelzaji wa miradi ya maendeleo.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akikagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk.Kalekwa Kasanga akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na matundu 12 ya vyoo katika shule ya Msingi Bugogo.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Bugogo kwenye Mkutano wa Hadhara.

Mbunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad akizungumza kwenye mkutano na wananchi wa Kijiji cha Bugogo.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela akizungumza.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza kwenye mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti wa Halamshauri ya wilaya ya Shinyanga Seth Msangwa akizungumza kwenye mkutano huo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464