Na Mwandishi wetu -
Uchaguzi Mkuu wa 2025 unakaribia, na kwa vijana, huu si wakati wa maneno mengi au siasa za vijiweni. Ni wakati wa kufanya maamuzi ya kimkakati kwa kuangalia maono yanayoweza kubadilisha maisha yetu. Kasi, uthubutu na maono haya ndiyo sasa yanatakiwa kuongoza kura yako.
Katika kipindi cha karibu miaka mitano ya uongozi wake, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameibuka kama kielelezo cha mafanikio ya Tanzania ya leo, akiongoza taifa kuelekea kile kinachoweza kuitwa 'Nchi ya Maziwa na Asali' taifa la fursa, ustawi, na amani.
Katika mkutano mkubwa uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi wa Sengerema na Buchosa, Mkoani Mwanza, Dkt. Samia aliweka wazi dira yake ya miaka mitano ijayo: kujenga taifa lenye huduma bora, uchumi jumuishi, na maendeleo ya watu wote. Hii ndio kauli ya kweli ambayo vijana wanatakiwa kuipima.
Mfano wa Mguso wa Moja kwa Moja:
• Ajira kupitia Kilimo na Uvuvi: Rais amesisitiza kwamba uchumi wa watu ndio moyo wa taifa. Katika Mwanza, sekta ya uvuvi imepata mapinduzi makubwa, Serikali imejenga vizimba 400 vya kufugia samaki, na wavuvi wamewezeshwa kwa boti na mikopo. Mabadiliko haya ni ajenda ya thamani inayolenga kuongeza kipato na kuchochea biashara moja kwa moja kwa vijana wanaotegemea sekta hizi
• Huduma Bora: Ameahidi kuimarisha afya, elimu, maji safi, nishati, na ajira. Hizi ndizo 'kwa nini' za msingi za vijana wanapaswa kupiga kura.
Kura Sio Jazba, Ni Ukomavu wa Kisiasa
Tanzania sasa ipo katika kipindi cha hamasa ya uchaguzi yenye utulivu. Tofauti na chaguzi za zamani, dalili zote zinaonyesha kuwa Watanzania wamefikia kiwango kipya cha uelewa wa kisiasa. Hakuna vurugu, hakuna hofu, bali kuna hamasa ya ushiriki.
Fanya Maamuzi ya Kimantiki, Si Kihisia
Kwa vijana, huu ni wakati wa kufanya maamuzi kwa mantiki, si kwa hisia.
Kama unataka:
• Kupunguza gharama za maisha.
• Kupata ajira za moja kwa moja kupitia miradi mikubwa.
• Kuona miradi inatekelezwa kwa kasi na ubora.
Basi unapaswa kupiga kura kwa kiongozi ambaye ameonesha uwezo wa kutafsiri ndoto kuwa matendo halisi. Kura yako inapaswa kuakisi rekodi ya uthabiti na matokeo, siyo porojo za kisiasa.