` MHE.SAMIA ATANGAZA MEMA KISHAPU

MHE.SAMIA ATANGAZA MEMA KISHAPU

Rais wa Awamu ya Sita na Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe.Samia Suluhu Hassan (kulia)akimkabidhi ilani ya chama hicho mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Lucy Thomas Mayenga(Kulia) Oktoba 11,2027  Kata ya Maganzo Wilayani Kishapu

Na Sumai Salum – Kishapu

Rais wa Awamu ya Sita na Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Samia Suluhu Hassan, ameanza rasmi ziara yake ya kuomba ridhaa ya wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 29,2025.

Akizungumza katika mkutano huo wa kampeni Leo Oktoba 11, 2025 katika eneo la Maganzo, Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi, Mhe. Samia amewapongeza wananchi wa Kishapu kwa mapokezi makubwa na yenye bashasha waliyomuonesha, akisema hali hiyo inaonesha imani kubwa waliyonayo kwa Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake.

 Rais wa Awamu ya Sita na Mgombea Urais Kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye mkutano wa kampeni Maganzo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 11,2025


Amesema Ilani ya CCM kwa miaka mitano ijayo imeweka kipaumbele katika kuboresha huduma za kijamii zikiwemo elimu, afya, maji na miundombinu ya barabara, ili kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na maendeleo.

“Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuboresha sekta ya elimu na afya, huku tukihakikisha huduma hizi zinamfikia kila mwananchi. Pia tumejipanga kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya Kolandoto – Mwangongo yenye urefu wa kilomita 54,” amesema Rais Samia.

Aidha, amewahakikishia wachimbaji wa madini ya almasi wa Kishapu kuwa Serikali itaendelea kuwaunga mkono kwa kuongeza zaidi idadi ya leseni za uchimbaji hatua itakayoongeza fursa za ajira na mapato ya wananchi.

Akizungumzia sekta ya Viwanda, Rais Samia ameahidi kufufua kiwanda cha Shireku kilichopo Mhunze ili kiweze kuanza uzalishaji upya na kuchangia katika uchumi wa wananchi wa Kishapu.

Rais Samia amehitimisha hotuba yake kwa kuwataka wananchi wote waende kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29, 2025, na kuwachagua viongozi bora watakaoendeleza jitihada za maendeleo nchini.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso naye amebainisha kuwa Serikali imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji mijini na vijijini katika Wilaya ya Kishapu, ikiwemo kuboresha upatikanaji wa maji safi kwa wananchi huku miradi mikubwa mitano ikiinufaisha Kishapu.

Nae Waziri wa Kilimo na Mhe.Hussein Bashe amesema zao la pamba limekuwa mhimili mkubwa wa maendeleo ya uchumi kwa wananchi wa Kishapu hivyo sekta hiyo inaendelea kuboreshwa huku bei ya pamba mwaka ujao ikitarajiwa kupanda na wakulima kunufaika zaidi.

Kwa upande wake, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Lucy Mayenga, mbali na kuipongeza serikali ya Awamu ya sita Kwa fedha nyingi za utekelezaji miradi mbalimbali amesisitiza umuhimu wa serikali kuendeleza miradi ya kilimo cha umwagiliaji ili kuinua kipato cha wananchi.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt.Asha-Rose Migiro akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais wa Chama hicho Mhe.Samia Suluhu Hassan Maganzo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 11,2025Waziri wa Maji Juma Aweso akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais wa Chama hicho Mhe.Samia Suluhu Hassan Maganzo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 11,2025Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais wa Chama hicho Mhe.Samia Suluhu Hassan Maganzo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 11,2025Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais wa Chama hicho Mhe.Samia Suluhu Hassan Maganzo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 11,2025Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) akizungumza kwenye mkutano wa Kampeni wa mgombea Urais wa Chama hicho Mhe.Samia Suluhu Hassan Maganzo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Oktoba 11,2025


























Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464