Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MGOMBEA Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Rais,Dkt Samia Suluhu Hassan,ameonyesha kufurahishwa na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga jinsi walivyojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wake wa kampeni wa kunadi sera na ilani ya CCM,ili siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29 wampigie kura nyingi za ushindi pamoja na Wabunge na Madiwani wote wa CCM.
Mkutano huo wa Kampeni umefanyika leo Oktoba 11,2025 katika Uwanja wa CCM Kambarage Mjini Shinyanga,ambapo Rais Samia aliwanadi Wagombea Ubunge katika Majimbo saba ya Uchaguzi Mkoani Shinyanga na Madiwani wote wa CCM.
Rais Samia,akizungumza kwenye mkutano huo,amesema aliyoingia uwanjani CCM Kambarage,hakuamini kama atakutana na umati mkubwa wa watu na kwamba angeambiwa leo afunge Kampeni zake basi angefungia Shinyanga kutokana na mapenzi makubwa ambayo wameonyesha wananchi wa Mkoa huo.
Aidha,amesema maendeleo ni safari,na kwamba kipindi cha miaka mitano iliyopita wamefanya mambo makubwa ya maendeleo na kuahidi kwamba kipindi kingine cha miaka mitano wanakwenda kufanya mambo makubwa ukiwamo mkoa huo wa Shinyanga.
Amesema kwa maombi mbalimbali ambayo yameombwa na Wagombea Ubunge na mengine ambayo hayapo kwenye Ilani ya CCM,kwamba ameyapokea na wataangalia uwezekano wa kuyafanyia kazi.
Pia,amewataka wananchi wa Mkoa huo wa Shinyanga Siku ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025 wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura na kumchagua awe Rais kwa miaka mitano tena.
TAZAMA PICHA👇👇
Mgombea Urais kupitia CCM Rais.Dk.Samia Suluhu Hassan akinda sera na ilani ya CCM kwa wananchi wa Shinyanga.
Mgombea Urais kupitia CCM Rais.Dk.Samia Suluhu Hassan akibidhi Ilani ya CCM kwa Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi.

Mgombea Urais kupitia CCM Rais.Dk.Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad.
Mgombea Urais kupitia CCM Rais.Dk.Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM,Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu Lucy Mayenga.