Suzy Butondo, Shinyangablog
Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga imefanya ziara ya kutembelea chuo cha Vijana Center kilichopo kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga kwa ajili yakuwapa elimu ya malezi bora ili waishi katika maadili mema ya kitanzania.
Ziara hiyo imeongozwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Fue Mrindoko ambaye alikuwa ameambatana na kamati yake ya utekelezaji ya wilaya ya Shinyanga mjini, ambapo amewataka wanafunzi wa chuo hicho kufuata malezi waliyoyapata kwa wazazi wao waache kuiga mambo ya mitandaoni ambayo yanasababisha mmomonyoko wa maadili.
"Tumekuja hapa kwa ajili ya kuwapa elimu ya malezi bora ambayo yatawasaidia kuishi vizuri hata mtakapomaliza masomo yenu ya chuo, achaneni na utandawazi wa mitandao ambao unaweza kubadili fikra zenu za maadili ya kiafrika shikeni elimu mnayofundishwa"amesema Mrindoko.
Katibu wa elimu na malezi Richard Mseti amewataka wanafunzi wa chuo hicho wasikubali kushawishika kuingia kwenye makundi maovu badala yake waendelee kuyaishi maadili waliyofundishwa na wazazi wao.
"Naomba niwashauri wanangu msikubali kushawishika kufanya mambo ya uovu ambayo hayampendezi Mungu hata mzazi pia fundishaneni maadilili mema na kuzingatia mnachofundishwa na walimu wenu ili mtakapomaliza muende mkautumie katika maisha yenu"amesema Mseti.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji Daniel Kapaya amewataka waachane na mawazo mabaya ambayo yanaweza kuwapelekea kufanya maovu, badala yake wakumbuke walichofundishwa na wazazi wao, na wasifanyiane ukatili,waishi katika maisha yaupendo na hofu ya Mungu.
"Baaddi ya watoto wamekuwa wakitoka kwa wazazi wao wakiwa namaadili mema lakini wakifika chuo wanabadilika , hivyo nnyinyi msifanye hivyo endeleeni kuwa na maadili yenu mliyofundishwa lakini pia muwe makini na mitandao ya kijamii kuna mambo mazuri lakini kuna
vitu vingine vinapotosha