` JUMUIYA YA WAZAZI SHINYANGA MJINI IMEFANYA ZIARA KATA YA KITANGILI YA KUWAOMBA WANANCHI WAJITOKEZE KUPIGA KURA OKTOBA 29, NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

JUMUIYA YA WAZAZI SHINYANGA MJINI IMEFANYA ZIARA KATA YA KITANGILI YA KUWAOMBA WANANCHI WAJITOKEZE KUPIGA KURA OKTOBA 29, NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

 



Suzy Butondo, Shinyangablog 

 Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini imefanya ziara katika kata ya Kitangili Shinyanga mjini na kukutana na makundi mbalibali ya bodaboda, timu za mpira wajasiliamali wa kilimo cha mboga mboga na baadhi ya mama lishe kwa ajili ya kuwaomba tarehe  29 mwezi huu wajitokeze kwa wingi  kuja kukipigia kura Chama Cha mapinduzi CCM.

 Ziara hiyo iliongozwa na mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mrindoko akiongozana na kamati ya utekelezaji ya jumuiya hiyo, mratibu wa kata hiyo Mwajuma Rabia   pamoja na mgombea udiwani wa kata hiyo Jonathan Madete.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Mrindoko amewaomba waendesha boda boda, wajasiliamali, mama lishe wanachama na wananchi wote wa kata ya Kitangili wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya kuwapigia kura wagombea wa CCM Rais Samia Suluhu, mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi na diwani wa kata ya ya Kitangili Jonathan Madete ili wapate kura za kishindo.

"Chama cha mapinduzi CCM kimefanya maendeleo makubwa katika kata yetu hii ya Kitangili na Taifa kwa ujumla tunayaona kwa macho kila sekta  hatusubiri kuambiwa, hivyo tunatakiwa tujitokeze wote tukawapigie kura wagombea wetu wa CCM ili waendelee kufanya makubwa zaidi"Mrindoko

Katibu wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Doris Kibabi amesema wamefanya ziara hiyo kwa lengo la kuhamasisha wanachama wananchi wote wa Kitangili wajitokeze kupiga kura, asitokee hata mmoja ambaye atapata udhuru siku hiyo wa kwenda kupiga kura.

Kwa upande wake mgombea udiwani kata ya Kitangili Jonathan Madete amewaomba wananchi, wajasiliamali boda boda, na mama lishe   wampigie kura nyingi za kishindo  mgombea Urais wa CCM, mbunge na yeye diwani  ili watakaposhinda waweze kuleta mabadiliko na kushirikiana nao ili kuwapatia mikopo yenye riba nafuu ili kila mmoja ajikwamue kiuchumi.

 "Niwaombe sana ndugu zangu mkiamini chama cha mapinduzi mjitokeze kwa wingi kutupigia kura, nawaahidi tutaboresha maisha   ya kila mmoja kwa kushirikiana nae na kuhakikisha anapata mkopo wa riba nafuu na kuondokana kausha damu ambayo imekuwa ikiwafanya wengi wateseke na kuishi bila amani katika familia zao"amesema Madete.

 Baadhi ya wajasiliamali wa mboga mboga wameiomba Jumuiya hiyo iwasaidie ili waweze kupata mbolea ya bei nafuu ili waweze kuweka kwenye  mashamba yao ya mbogamboga na dawa za kupulizia kwani  kuna wadudu wanakula mboga hizo, na waweze kusaidiwa ili nao wapatiwe fedha za halmashauri ambazo hazina riba ya kumuumiza 
mjasiliamali.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga Fue Mrindoko akizungumza na waendesha bodaboda viongozi wa timu za mpira wajasiliamali wa mbogamboga  na mama lishe 

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Shinyanga mjini Doris Kibabi akizungumza na waendesha bodaboda viongozi wa timu za mpira wajasiliamali wa mbogamboga  na mama lishe




Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Shinyanga mjini Doris Kibabi akitoa maelekezo ya kupigia kura wagombea  kwa waendesha bodaboda viongozi wa timu za mpira wajasiliamali wa mbogamboga  na mama lishe



















Mgombea Udiwani kata ya Kitangili Jonathan Madete akizungumza na wananchi wa kata hiyo













Mgombea Udiwani kata ya Kitangili Jonathan Madete akizungumza na wananchi wa kata hiyo














Mratibu wa kata ya Kitangili Mwajuma Rabia akizungumza na wananchi wa kata ya Kitangili 

















Katibu wa Jumuiya ya Wazazi Shinyanga mjini Dorisi Kibabi akisaidiana na wajasiliamsli wa kulima mboga mboga kuchambua 




Mgombea udiwani wa kata ya Kitangili Jonathan Madete akisaidiana na wajasiliamali wa kulima mboga mboga kuchambua 



Katibu wa jumuiya ya Wazazi akipumuzika baada ya Kuchimba Molamu katika kata ya Kitangili, ilikuwa kazi kweli kweli 

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464