Na Marco Maduhu,SHINYANGA
KOCHA wa Timu ya Pamba Jiji ambayo inashiriki kucheza msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2025/2026, Francis Baraza, amesema Stand United wana timu nzuri, na wakipata "Support": watafanya vizuri katika Ligi ya Championship na kurejea ligi kuu.
Amebainisha hayo leo Oktoba 4,2025 mara baada ya kuamalizika kwa mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Timu ya Stand United katika Tamasha la Siku ya Wana lililofanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage pamoja na kutambulishwa wachezaji wapya wa Stand United.
Amesema mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa na kila Timu imeonyesha ubabe wake,na kwamba ameiona Timu ya Stand United namna ilivyocheza kuwa ni Timu nzuri na wanawachezaji ambao wanauzoefu na wamewahi kucheza katika Timu kubwa.
“Timu ya Stand United ni nzuri,inachohitaji ni Support tu kutoka kwa mashabiki wao na wadau wa mpira ili iweze kufanya vizuri zaidi na kurejea ligi kuu,”amesema Baraza.
Kocha wa Timu ya Stand United Idd Cheche,amesema Timu yao ni nzuri ila bado kuna changamoto ndogo ambazo ameziona dhidi ya mchezo wao na Pamba Jiji, na kwamba watarudi katika uwanja wa mazoezi kuzifanyia kazi,na kwamba kabla ya kuanza ligi ya Championship watakuwa imara zaidi.
“Mapugufu ambayo nimeyaona siyo mengi,kuna makosa madogo madogo ambayo tunakwenda kuyarekebisha na tutafanya vizuri,”amesema Cheche.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro ambaye ni mlezi wa Timu ya Stand United,anasema kikosi walichonacho ni kizuri zaidi kulika msimu uliopita na kwamba msimu huu wa Champioship lazima warejee ligi kuu.
Amesema,wataendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo ili kuinga mkono timu hiyo na iweze kusonga mbele na kwamba msimu huu watapita moja kwa moja kushiriki ligi kuu na hakuna tena kucheza playoff.
Aidha,katika Mchezo huo Stand United na Pamba Jiji hadi dakika 90 zinamalizika walitoka bila ya kufungana.
TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro ambaye ni mlezi wa Timu ya Stand United akizungumza.
Kocha wa Pamba Jiji Francis Baraza akizungumza.
Kocha wa Timu ya Stand United Idd Cheche akizungumza.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464