

Suzy Butondo, Shinyanga
Katibu mkuu wa Jumuiya ya Wazazi
Taifa Ally Hapi amefanya ziara mkoani Shinyanga ya
kuhamasisha wananchi wajitokeze kupiga kura oktoba 29 mwaka huu,ambapo
amewaomba wampigie kura mgombea Urais wa CCM Samia Suluhu,wabunge
na madiwani wote wa Chama hicho,
Hayo ameyasema wakati akizungumza na wananchi wa jimbo
la Itwangi Mkoani Shinyanga, amesema Chama Cha mapinduzi CCM kwa
kusimamiwa na Rais Samia Suluhu imejipanga vizuri kuhakikisha iinainua
maisha ya kila mtanzania, hivyo amewaomba kuwapa ridhaa tena.
Hapi amesema ilani ya Chama
Cha Mapinduzi CCM iliyopita imetekelezwa kikamilifu , lakini ilani
ya sasa imesheheni mambo makubwa zaidi kuliko ilani iliyopita kwa ajili
ya maendeleo ya wananchi, ili kuhakikisha kila mmoja anainuka kiuchumi.
"Niwaombe sana wananchi wa mkoa
wa Shinyanga mjitokeze wote kupiga kura mkipigie chama cha Mapinduzi CCM kwa
sababu kimesimamia ilani ya CCM,na awamu hii ilani yetu imesheheni
mipango mikubwa na tunasema ilani hii kama ni Ng"ombe ni Nzagamba,"amesema
Hapi


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Mkoa
wa Shinyanga John Siagi amewaomba wananchi wote wajitokeze kupiga kura ili
wakichague chama cha Mapinduzi kwa sababu kina ilani iliyosheni mipango ya
kuwasaidia wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi
Taifa ameongozana na timu yake ambapo amefanya mikutano katika Kata ya Samuye,
Mwamala, Usule kisha baadhi ya viongozi wa Jumuiya hiyo kumwakilisha kutano wa
Tinde baada ya kupata dharura ya kikazi.













