` SHYDC WAJIVUNIA SHULE YA AWALI NA MSINGI OLA KUFANYA VIZURI KITAALUMA

SHYDC WAJIVUNIA SHULE YA AWALI NA MSINGI OLA KUFANYA VIZURI KITAALUMA


SHYDC WAJIVUNIA SHULE YA AWALI NA MSINGI OLA KUFANYA VIZURI KITAALUMA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

AFISA Elimu wa Shule za Msingi Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Andrew Mitumba,amesema wanajivunia Shule ya Awali na Msingi OLA,kutokana na kufanya vizuri kitaaluma na kufaulisha wanafunzi katika Mitihani ya Kitaifa ikiwamo ya darasa la Saba.

Amebainisha hayo leo Oktoba 4,2025 kwenye Mahafali ya pili ya wanafunzi wa Awali, na ya Tano ya darasa la 7 katika shule hiyo.
Mitumba akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, amesema shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri Kitaaluma na kutoa elimu bora kwa wanafunzi na malezi mema yenye maadili na kwamba wanajivunia uwepo wa shule hiyo wilayani Shinyanga.

"Shule hii ya Msingi OLA sisi kama Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, tunajivunia sana sababu kila mwaka imekuwa ikifanya vizuri kitaaluma na kufaulisha wanafunzi wote wa darasa la Saba kwa ufaulu wa juu kabisa,"amesema Mitumba.

Aidha,amesema wanaipongeza pia shule hiyo kwa matumizi ya nishati safi ya kupikia na kumuunga mkono Rais Dk.Samia Suluhu Hassan katika mkakati wake wa utunzaji wa mazingira katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Naye Mkuu wa Shule hiyo Sister Comfort Amevor,ametoa wito kwa wazazi kwamba wahitimu hao watakapo kuwapo majumbani wakisubili matokeo, wawa tunze katika malezi mema na yenye maadili kama walivyokuwa wakitunzwa shuleni hapo.

Ametoa wito pia kwa wahitimu hao,kwamba watakapo anza masomo ya kidato cha kwanza ,waendelee na kasi ile ile ya kujisomea ili wafanye vizuri kitaaluma na kutimiza ndoto zao na kuwa mabalozi wazuri wa shule hiyo ya OLA.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa shule ya Awali na Msingi OLA Yohana Shija, ametaja idadi ya wanafunzi ambao wamehitimu darasa la Saba kuwa ni 33 wavulana 16 na wasichana17 na Wahitimu darasa la Awali kuwa ni 55,wavulana 28 na wasichana 27.

Nao baadhi ya wazazi,wamepongeza utoaji wa taaluma bora katika shule hiyo, huku wakiahidi kuendelea kusomesha watoto na kutimiza ndoto zao.

TAZAMA PICHA👇👇
AFISA Elimu wa Shule za Msingi Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Andrew Mitumba akizungumza kwenye mahafali hayo.
Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi OLA Sister Comfort Amevor akizungumza kwenye mahafali hayo.
Makamu Mkuu wa shule ya Awali na Msingi OLA Yohana Shija akisoma taarifa ya shule.






Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464