` UDHAMINI WA KIHISTORIA! JAMBO GROUP YAIPA NGUVU DODOMA JIJI FC LIGI KUU TANZANIA BARA

UDHAMINI WA KIHISTORIA! JAMBO GROUP YAIPA NGUVU DODOMA JIJI FC LIGI KUU TANZANIA BARA

Viongozi wa Jambo Group na Dodoma Jiji FC wakisaini mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/2026, katika hafla iliyofanyika Ibadakuli, Shinyanga. Viongozi wa Jambo Group na Dodoma Jiji FC wakizindua rasmi jezi ya timu hiyo yenye chapa ya mdhamini mpya, Jambo Group ‘Jamukaya’, katika hafla ya kusaini mkataba wa udhamini jijini Shinyanga.
Familia mpya ya Jamukaya! Viongozi wa Jambo Group na Dodoma Jiji FC wakipiga picha ya pamoja baada ya kusaini mkataba wa udhamini wa Ligi Kuu msimu wa 2025/2026.

Na Kadama Malunde – Shinyanga

Kampuni ya Jambo Food Products imeendelea kuonesha mchango wake mkubwa katika kukuza michezo nchini baada ya kutangaza rasmi kudhamini klabu ya Dodoma Jiji FC inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2025/2026.

Mkataba huo wa mwaka mmoja umesainiwa Septemba 23, 2025 kati ya viongozi wa Jambo Food Products na Dodoma Jiji FC, katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Kata ya Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga.

Akizungumza wakati wa utiaji saini, Msimamizi wa Chapa na Ubunifu wa Jambo Group, Nickson George, amesema kampuni hiyo imeendelea kuzisaidia timu mbalimbali nchini, na sasa imeamua kushika mkono Dodoma Jiji FC ili kufanikisha ndoto na malengo yao kwenye Ligi Kuu.

“Hatua hii siyo tu udhamini, bali ni ushirikiano wa kibiashara na kijamii utakaosaidia kukuza chapa za pande zote mbili kupitia michezo. Dodoma Jiji FC sasa ni sehemu ya familia ya Jambo Group – ‘Jamukaya’, na Jambo Group ni sehemu ya Dodoma Jiji FC,” amesema George.

Kwa upande wake, Kiongozi wa Dodoma Jiji FC, Dickson Kimaro, ameishukuru Jambo Group kwa kuiamini timu yao na kuahidi kuitangaza vyema chapa ya kampuni hiyo kupitia matokeo mazuri katika msimu huu wa ligi.
Kiongozi wa Dodoma Jiji FC, Dickson Kimaro, akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa udhamini na Jambo Group, Shinyanga. Kulia ni Msimamizi wa Chapa na Ubunifu wa Jambo Group, Nickson George.

“Kwa niaba ya halmashauri ya Jiji la Dodoma, mashabiki na viongozi wa timu yetu, tunashukuru sana kwa heshima hii kubwa. Tunaahidi kushirikiana vyema na kuhakikisha tunatoa matokeo chanya uwanjani,” amesema Kimaro.

Hii si mara ya kwanza kwa Jambo Group kuwa mdau wa soka nchini. Septemba 13, 2025 kampuni hiyo pia ilitangaza kuwa mdhamini mkuu wa Pamba FC ya Mwanza, na awali imewahi kudhamini timu nyingine kubwa za Kanda ya Ziwa ikiwemo Stand United ya Shinyanga.

Kwa hatua hizi, Jambo Group inaendelea kuthibitisha nafasi yake kama mdhamini kinara wa soka la Tanzania, hususan kwa klabu zinazopanda chati na kuonesha ushindani kwenye Ligi Kuu.
Msimamizi wa Chapa na Ubunifu wa Jambo Group, Nickson George, akizungumza katika hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa udhamini kati ya Jambo Group na Dodoma Jiji FC. Picha na Kadama Malunde
Msimamizi wa Chapa na Ubunifu wa Jambo Group, Nickson George, akifafanua umuhimu wa udhamini huo kwa pande zote mbili wakati wa hafla ya kusaini mkataba na Dodoma Jiji FC.
Msimamizi wa Chapa na Ubunifu wa Jambo Group, Nickson George, akizungumza katika hafla fupi ya utiaji saini wa mkataba wa udhamini kati ya Jambo Group na Dodoma Jiji FC.
Kiongozi wa Dodoma Jiji FC, Dickson Kimaro, akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa udhamini na Jambo Group, Shinyanga.
Kiongozi wa Dodoma Jiji FC, Dickson Kimaro, akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba wa udhamini na Jambo Group, Shinyanga.
Viongozi wa Jambo Group na Dodoma Jiji FC wakizindua rasmi jezi ya timu hiyo yenye chapa ya mdhamini mpya, Jambo Group ‘Jamukaya’, katika hafla ya kusaini mkataba wa udhamini jijini Shinyanga.

Viongozi wa Jambo Group na Dodoma Jiji FC wakisaini mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/2026, katika hafla iliyofanyika Ibadakuli, Shinyanga.
Viongozi wa Jambo Group na Dodoma Jiji FC wakionesha nakala ya mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/2026, mara baada ya hafla ya utiaji saini iliyofanyika Ibadakuli, Shinyanga.
Viongozi wa Jambo Group na Dodoma Jiji FC wakibadilishana nakala ya mkataba wa mwaka mmoja wa udhamini wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/2026, mara baada ya hafla ya utiaji saini iliyofanyika Ibadakuli, Shinyanga.
Picha ya pamoja ya viongozi wa Jambo Group na Dodoma Jiji FC baada ya kusaini mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Viongozi wa Jambo Group na Dodoma Jiji FC wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusainiwa kwa mkataba wa udhamini wa mwaka mmoja wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/2026, Ibadakuli – Shinyanga.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464