` SHIRIKA LA YAWE KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA KUZIJENGEA UWEZO KAMATI ZA MAZINGIRA KATA TATU SHINYANGA

SHIRIKA LA YAWE KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI KWA KUZIJENGEA UWEZO KAMATI ZA MAZINGIRA KATA TATU SHINYANGA

Afisa Miradi wa Mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kutoka Shirika la YAWE Peter Nampala akizungumza wakati wa mafunzo kwa wajumbe wa kamati za mazingira kutoka Kata ya Ndala na Masekelo

Na Stella Herman,Shinyanga

Shirika la YAWE limeanza kutoa mafunzo kwa wajumbe wa kamati za mazingira Kata ya Ndala na Masekelo Manispaa ya Shinyanga ili kuwawezesha kwenda kusimamia vizuri uhifadhi wa mazingira kwa kuzingatia kanuni,miongozo na sheria wanapokuwa wanatekeleza majukumu yao.

Hayo yameelezwa leo na Peter Nampala ambaye ni Afisa Miradi wa Mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kutoka Shirika la YAWE  linalojihusisha na masuala ya usawa wa kijinsia, ulinzi wa Mtoto, Afya na Lishe, Mazingira na mabadiliko ya Tabia nchi pamoja na Demokrasia na Utawala wakati wa mafunzo kwa wajumbe wa kamati za mazingira kutoka Kata ya Ndala na Masekelo.

Amesema uharibifu wa mazingira umekuwa ukisababisha athari kubwa nchini na ndiyo maana wameamua kuzihuhisha kamati hizo na kuziwezesha kwenda kutekeleza majukumu yao ipasavyo katika kusimamia suala la mazingira.

“Mafunzo haya yamelenga kuwafikia wanakamati hao ambapo wamezingatia makundi mbalimbali wakiwemo wanawake,wanaume na watu wenye ulemavu kutoka Kata za Masekelo na Ndala na tunatarajia tukimaliza Kata hizo tutaanza kutekeleza mradi huo Kata ya Mwawaza ambapo lengo la mradi ni kufikia Kata hizo tatu”, amesema Peter.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya maliasili na hifadhi ya mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga

Kwa upande wake Mwezeshaji wa mafunzo hayo ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya maliasili na hifadhi ya mazingira Manispaa ya Shinyanga Ezra Manjerenga amesema kupitia mafunzo hayo wanatarajia kuona usimamizi mkubwa wa sheria ya mazingira ya mwaka 2004 ili kuyalinda na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Amesema kamati hizo zinakwenda kufanya kazi kwa kuwashirikisha wananchi kuanzia ngazi ya chini ili kuhakikisha kunakuwa hakuna uharibufu wa mazingira unaofanywa hatua ambayo itawezesha kutunza mazingira,

Amesema anaamini Kata ya Masekelo na Ndala ambapo mradi huo unatekelezwa watakuwa mfano katika utunzaji wa mazingira ili kuviwezesha vizazi vijavyo kuwa katika mazingira mazuri.
Afisa Miradi wa Mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi kutoka Shirika la YAWE Peter Nampala
Mafunzo yanaendelea
Wajumbe wa Kamati za Mazingira
Washiriki wakifuatilia mafunzo
Mafunzo yanaendelea

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464