` PROGRAMU ZA MAFUNZO KWA VITENDO ZA BARRICK ZAENDELEA KUNUFAISHA WANAFUNZI WA VYUO VYA KATI NA ELIMU YA JUU NCHINI

PROGRAMU ZA MAFUNZO KWA VITENDO ZA BARRICK ZAENDELEA KUNUFAISHA WANAFUNZI WA VYUO VYA KATI NA ELIMU YA JUU NCHINI

 


Baadhi ya Wanafunzi waliopo kwenye mafunzo katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Barrick North Mara
Baadhi ya Wanafunzi waliopo kwenye mafunzo 
Baadhi ya Wanafunzi waliopo kwenye mafunzo

***
Kutokana na serikali kufungua milango ya wawekezaji wakubwa kwenye sekta mbalimbali nchini na kasi ya mabadiliko ya matumizi ya sayansi na teknolojia kunahitajika jitihada za maksudi za kuhakikisha watanzania wananufaika na uwekezaji huo kikamilifu.

Uwekezaji wa kweli sio tu wa fedha na teknolojia bali kunahitajika kuwekeza katika kuinua na kuendeleza vipaji ili kupata wataalamu wenye weledi wa kuweza kushiriki kuendesha miradi inayofunguliwa na wawekezaji kwa kipindi cha sasa na siku za usoni ili kunufaika na uwekezaji huo.

Moja ya kampuni kubwa iliyowekeza nchini katika sekta ya madini ambayo mbali na kujikita kuwekeza katika fedha na matumizi ya teknolojia za kisasa inawekeza katika kuboresha elimu nchini,kuinua vipaji vya vijana wa kitanzania ni Barrick ambayo kwa hapa nchini inaendesha shughuli zake kwa ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals.

Kupitia progamu ya kuwapatia mafunzo ya vitendo (Practical training) na mifumo thabiti kutokana na uwekezaji makini na sera zenye mtazamo wa kujenga jamii endelevu . Kila mwaka migodi ya Barrick ya Bulyanhulu na North Mara imekuwa ikitoa nafasi kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaosoma vyuo vikuu vya hapa nchini katika fani mbalimbali kupata mafunzo ya vitendo.
Wanafunzi wa vyuo vya elimu wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo kutoka kwa wafanyakazi wa Barrick wakati wa makongamano ya kuwajengea uwezo kupitia taasisi ya AIESEC Tanzania mwaka huu.

Mbali na programu hiyo pia Barrick inayo programu ya kutoa mafunzo ya vitendo kwa wanafunzi waliohitimu vyuo vikuu na vya kati (internship) kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo wahitimu waliochaguliwa hupata fursa ya kufanya kazi na timu ya wafanyakazi wa kampuni waliobobea katika fani mbalimbali na kupata maarifa sambamba na kugharamiwa gharama za kujikimu na zijitokezapo fursa baadhi yao hujipatia ajira za kudumu kwenye migodi hiyo.

Vilevile Barrick inayo programu ya kuwanoa vijana wasomi kupata ujuzi na uzoefu zaidi wahitimu hususani katika sekta ya madini (Graduate Programme) ambapo hujengewa uwezo kwa kipindi cha miaka mbili kwa kufanya kazi kwa karibu na wataalamu wa kampuni na baada ya kipindi hicho baadhi yao hupatiwa ajira ndani ya kampuni na wengine kuruhusiwa kutafuta ajira katika sehemu nyinginezo.

Kampuni ya Barrick pia inayo programu ijulikanayo kama First Entry ambayo imelenga kuwanufaisha vijana wanaotoka kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi wasio na ujuzi wowote ambapo baadhi yao hubahatika kupatiwa mafunzo ya aina mbalimbali migodini na pindi wamalizapo hupatiwa ajira za kudumu na wengine hutumia ujuzi walioupata kupata kazi kwenye maeneo mengine.
Katika miaka ya karibuni pia Barrick nchini imekuwa kinara wa kudhamini makongamano ya wanafunzi wa vyuo vya juu na vya kati nchini kupitia taasisi ya AIESEC ambapo pia wafanyakazi wa Barrick waliobobea katika fani mbalimbali wamekuwa wakishiriki na kuwajengea uwezo wanafunzi kuhusu kujiandaa kwa siku zijazo na jinsi ya kukabiliana na changamoto na jinsi ya kutumia elimu na vipaji vyao kujiendeleza kimaisha sambamba na utambuzi wa fursa mbalimbali za ajira na kujiajiri.

Akiongea wakati wa kutoa muhtasari wa yaliyomo katika ripoti mpya ya utekelezaji wa mkakati endelevu ya Barrick ya mwaka jana karibuni,Rais na Afisa Mtendaji Mkuu wa Barrick,Mark Bristow alibainisha mafanikio makubwa yaliyopatikana kutokana na kampuni kutekeleza malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) kwa vitendo mojawapo ikiwa ni kuboresha elimu kupitia uwekezaji wake katika sehemu mbalimbali duniani.

Pia alipokuwa kwenye ziara ya kikazi nchini karibuni alisema Barrick inalipa umuhimu mkubwa suala la elimu na itaendelea kuwekeza katika sekta hiyo ili kuhakikisha watanzania wanapata elimu na ndio maana inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kuboresha mazingira ya kutoa elimu bora nchini.

Baadhi ya Wanafunzi waliopo katika mafunzo ya vitendo walipohojiwa kuhusiana na kupata fursa ya mafunzo ya vitendo katika migodi ya Barrick walisema kinachowafurahisha na kujengewa uwezo na wafanyakazi wenye weledi mkubwa, kuona kampuni inayapa kipaumbele masuala ya msingi katika kujenga biashara endelevu kama vile utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji, usalama wa wafanyakazi wake ,kushirikiana na jamii zilizopo katika maeneo inakofanyia biashara zake, kufanikisha miradi mbalimbali ya kusaidia jamii hususani katika sekta ya elimu,afya na miundombinu.
Wanafunzi wa vyuo vya elimu wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo kutoka kwa wafanyakazi wa Barrick wakati wa makongamano ya kuwajengea uwezo kupitia taasisi ya AIESEC Tanzania mwaka huu.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464