` MKOPO KWA WAKULIMA KUTOKA NMB KISHAPU WAWAPA KICHEKO WAKULIMA KWA KUPATA MATREKTA

MKOPO KWA WAKULIMA KUTOKA NMB KISHAPU WAWAPA KICHEKO WAKULIMA KWA KUPATA MATREKTA

 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi (kushoto) na Meneja wa Benki ya NMB Wilayani humo Alexander Macheko (kulia) wakati Mkuu wa Wilaya akikabidhi Kwa wakulima wanne matrekta yenye thamani ya Tsh. 238,400,000 Kwa mkopo kutoka Banki ya NMB Wilayani humo kwa ajili ya shughuli za kilimo Septemba 25,2025

Na Sumai Salum – Kishapu

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, amewakabidhi wakulima wanne Wilayani humo matrekta yenye thamani ya Shilingi 238,400,000/=, yaliyopatikana kupitia mkopo nafuu kutoka Benki ya NMB.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika Septemba 25, 2025, katika viwanja vya Benki ya NMB Wilayani humo Masindi amesema hatua hiyo ni chachu ya kuwaletea wamiliki wa matrekta hayo ongezeko la kiuchumi kupitia kilimo cha kisasa.Meneja Benki ya NMB Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Alexander Macheko akizungumza wakati Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Peter Masindi akikabidhi Kwa wakulima wanne matrekita yenye thamani ya Tsh. 238,400,000 Kwa mkopo kutoka Banki ya NMB Wilayani humo Septemba 25,2025

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia NMB imetoa mikopo kwa riba nafuu ya asilimia 9. Tuyatumie kwa malengo ya kuongeza kipato cha familia huku mkikumbuka kurejesha mikopo hiyo kwa mujibu wa mkataba,” amesema Masindi.

Ameongeza kuwa serikali ya Awamu ya Sita inatambua thamani ya mkulima kwa kuwa sekta ya kilimo ni mhimili wa pato la taifa, na hivyo wamiliki wa matrekta wanapaswa kuwa mfano wa kuhamasisha matumizi ya teknolojia badala ya kilimo cha jembe la mkono na kutumia mifugo.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi(katikati),Meneja Mwandamizi wa Mauzo ya bidhaa za kidgitali NMB Makao makuu(kushoto) na Meneja wa Benki ya NMB Wilayani Kishapu Alexander Macheko baada ya Mkuu huyo wa Wilaya kuwaabidhi Wakulima Wanne matrekta ya kulimia yenye thamani ya Tsh.238,400,000 Septemba 25,2025

Aidha, amewataka wamiliki wa matrekta hayo kuwashirikisha vijana kwa kuwaelezea faida za kilimo cha kisasa kupitia zana hiyo ili nao watumie fursa hiyo kujikwamua kiuchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga akizungumza wakati akikabidhi matrekta manne Kwa wakulima wanne yenye thamani ya Tsh.238,400,000 Septemba 25,2025 kwenye Viwanja vya Banki ya NMB tawi la Kishapu

“Vijijini mnakokaa tangazeni huduma za kulima kwa trekta. Wakulima watawafuata, ninyi mtaongeza kipato, familia zenu zitapata nafuu na marejesho ya mkopo hayatakuwa kikwazo,” amesisitiza

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi (kushoto) akiwa na Meneja wa Banki ya NMB Wilayani humo Alexander Gabriel Macheko Septemba 25,2025 wakati Mkuu huyo akikabidhi Matrekta manne kwa wakulima wananne walionufaika na mkopo kutoka Benki ya NMB 

Kwa upande wake, Meneja wa Banki ya NMB Wilayani humo Alexander Gabriel Macheko, amesema lengo la kutoa mikopo hiyo ni kusaidia kuinua sekta ya kilimo na kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi.

“Tunaamini wamiliki hawa wanne watahamasisha jamii zao kuhusu urahisi na faida ya kutumia trekta. NMB pia inatoa mikopo kwa wafugaji wanao nenepesha mifugo, wajasiriamali wadogo ili kuinua biashara zao na watumishi wapya ambao hawajathibitishwa kazini, ili kuchochea maendeleo ya kiuchumi,” amesema Macheko.
Picha ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi(watatu kutoka kushoto) akiwa na wakulima wanne kutoka Wilayani humo baada ya kuwakabidhi matrekta kwa ajili ya shughuli za kilimo Septemba 25,2025

Nao wakulima walionufaika na mkopo huo akiwemo Sagala Luminu, Magida Luahu, Saba Kwihula na Machiya Mhuli, wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutambua mchango wa wakulima, wakibainisha kuwa mikopo hiyo yenye masharti nafuu itawaondolea changamoto ya muda mwingi ambapo awali walikuwa wakitumia jembe la mikono na mifugo kama Punda na Ng'ombe na sasa itawasaidia kuongeza tija kwenye kilimo.
Mkuu wa Wilaya Mhe.Peter Masindi akikabidhi ufunguo wa trekta kwa Mkulima Septemba 25,2025
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464