` MAYENGO : OKTOBA TUNATIKI KWA DKT. SAMIA, AZZA HILLAL

MAYENGO : OKTOBA TUNATIKI KWA DKT. SAMIA, AZZA HILLAL

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Simon Makoye Mayengo akizungumza katika mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Mkoani Shinyanga- Picha na Kadama Malunde
Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Simon Makoye Mayengo akizungumza katika mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Mkoani Shinyanga
Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Simon Makoye Mayengo akizungumza katika mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Mkoani Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mjumbe wa Kamati ya Siasa CCM Mkoa wa Shinyanga, Ndg. Simon Makoye Mayengo, amesema wananchi wa Jimbo la Itwangi wanapaswa kuendeleza imani yao kwa CCM, kwani chama kimeleta wagombea wanaouzika, makini na mbobevu.

Akizungumza katika mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Mkoani Shinyanga Mhe. Azza Hillal Hamad uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi amesema wagombea wa CCM wana sifa zote za uongozi hivyo hawana mashaka na ushindi wa CCM.

"Kama Mlezi wa Jimbo la Itwangi, tunamshukuru sana Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kutuletea mgombea wetu makini ambaye ni mbobevu katika nafasi hii, alipumzika kidogo na sasa anaenda kuleta maendeleo ya Jimbo Jipya la Itwangi. Oktoba tunatiki kwa Azza Hillal Hamad na Dkt. Samia Suluhu Hassan na Madiwani wa CCM," amesema Mayengo.

Akizungumza katika mkutano wa Uzinduzi wa Kampeni za Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi, Mayengo amesema wagombea wa CCM wana sifa zote za uongozi hivyo hawana mashaka na ushindi wa chama.

"Kama Mlezi wa Jimbo la Itwangi, tunamshukuru sana Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kutuletea mgombea wetu makini ambaye ni mbobevu katika nafasi hii, alipumzika kidogo na sasa anaenda kuleta maendeleo ya Jimbo Jipya la Itwangi. Oktoba tunatiki kwa Azza Hillal Hamad na Dkt. Samia Suluhu Hassan na Madiwani wa CCM," amesema Mayengo.

Akihutubia wananchi, Mhe. Azza Hillal Hamad amewaahidi maendeleo endapo atapewa ridhaa ya kuongoza Itwangi, akitaja miradi ya maji, afya, elimu na umwagiliaji kuwa kipaumbele chake. Ameahidi kuhakikisha skimu za umwagiliaji ikiwemo Nyida na nyingine ambazo hazijakamilika zinakamilishwa, pamoja na miradi ya maji ikiwemo ule wa Ziwa Victoria na ule wa Tinde Package ili vijiji vyote vipate huduma.

"Wananchi wa Itwangi, Oktoba 29 nikopesheni imani niwatumikie. Hakuna chama kingine kinachoweza kuwaletea maendeleo zaidi ya CCM," amesema Azza. Pia amemtaja Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama kiongozi mwenye dira, akieleza jinsi alivyopeleka miradi mikubwa ya kimkakati Itwangi, ikiwamo Reli ya Kisasa (SGR), miundombinu ya barabara, elimu, afya na skimu za umwagiliaji.

Uzinduzi huo uliofanyika kwa shamrashamra kubwa umehudhuriwa na wananchi, wanachama wa CCM, wagombea udiwani pamoja na viongozi mbalimbali wa chama, huku Munde Tambwe Abdallah, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), akiwa mgeni rasmi.

Akizungumza, Munde ameeleza kuwa Azza ni Mbunge Jembe mwenye uwezo mkubwa wa kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo.

"Azza ni chaguo sahihi. Ni jasiri, mjenga hoja na mtetezi wa wananchi. Nawaomba Oktoba 29 mpigie kura Rais Dkt. Samia, Azza Hillal na madiwani wote wa CCM ili tuendelee kupata maendeleo," amesema Munde.

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Munde Tambwe Abdalla akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Itwangi
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Munde Tambwe Abdalla akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Itwangi
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akiwaombea kura wagombea udiwani kata za Jimbo la Itwangi

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464