` MAHAFALI YA KWANZA CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA KAMPASI YA SHINYANGA YAFANYIKA,WAHITIMU KUPEWA KIPAUMBELE CHA AJIRA

MAHAFALI YA KWANZA CHUO CHA SERIKALI ZA MITAA KAMPASI YA SHINYANGA YAFANYIKA,WAHITIMU KUPEWA KIPAUMBELE CHA AJIRA


Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MAHAFALI ya kwanza ya Chuo cha Serikali za Mitaa Kampasi ya Shinyanga yamefanyika leo Desemba 19, 2025, ambapo serikali imesema itaendelea kutoa kipaumbele cha ajira kwa wahitimu wa chuo hicho wanaokidhi vigezo vya ajira, katika nafasi za ajira zinazotolewa na mamlaka za serikali za mitaa.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dk. Jafar Seif, alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo akimwakilisha Waziri wa TAMISEMI, Profesa Riziki Shemdoe.

Dk. Seif amesema kufunguliwa kwa kampasi hiyo mkoani Shinyanga ni hatua muhimu katika kusogeza elimu karibu na wananchi, huku akisema anayofuraha kutunuku vyeti kwa wahitimu katika mahafali yao ya kwanza, na kwamba katika nafasi za ajira za serikali za mitaa zitakazo kuwa zikitoka watapewa kipaumbele wanaokidhi vigezo.
“Natoa wito kwa wahitimu kuwa waadilifu, wazalendo wa taifa lao, wachapakazi, wenye nidhamu na kutumia utaalamu na weledi walioupata katika kuwatumikia wananchi,” amesema Dk.Seif.

Awali, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dk. Mashala Yusuph, akisoma risala ya chuo, amesema jumla ya wanachuo 350 wamehitimu katika kozi mbalimbali.
Amesema chuo hicho kitaendelea kuzalisha wataalamu waliobobea, wenye uwezo mkubwa wa kiutendaji na wanaokidhi mahitaji ya utumishi katika mamlaka za serikali za mitaa.

Kwa upande wao, baadhi ya wahitimu wameishukuru serikali kwa kufungua kampasi hiyo mkoani Shinyanga, hatua iliyowawezesha kupata elimu karibu na maeneo yao, tofauti na awali walipolazimika kusoma mkoani Dodoma.
Wameahidi kuwa watumishi waadilifu, wachapakazi na waaminifu pindi watakapopata ajira serikalini.

TAZAMA PICHA👇👇
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dk. Jafar Seif akizungumza katika mahafali ya kwanza Chuo cha Serikali za Mitaa Kampasi ya Shinyanga.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dk. Jafar Seif, akizungumza katika mahafali ya kwanza Chuo cha Serikali za Mitaa Kampasi ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akizungumza.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Serikali za Mitaa, Dk. Mashala Yusuph akisoma risala katika mahafali hayo.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dk. Jafar Seif, akitunuku vyeti vya pongezi kwa wahitimu waliofanya vizuri kitaaluma
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464