` MALUNDE AMUOMBEA KURA DKT. SAMIA, AZZA HILLAL

MALUNDE AMUOMBEA KURA DKT. SAMIA, AZZA HILLAL

Aliyekuwa Mtia Nia ya Ubunge Jimbo la Itwangi Mhandisi Sebastian Malunde , akiwaombea kura wagombea wa CCM kwenye  uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Itwangi - Picha na Malunde 1 blog
Aliyekuwa Mtia Nia ya Ubunge Jimbo la Itwangi Mhandisi Sebastian Malunde , akiwaombea kura wagombea wa CCM kwenye  uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Itwangi

Na Mwandishi Wetu, Shinyanga

Aliyekuwa Mtia Nia ya Ubunge Jimbo la Itwangi Mhandisi Sebastian Malunde , ameshiriki katika uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Itwangi, akiwaomba wananchi kumpa kura ya kishindo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hillal Hamad na madiwani wote wa CCM.

Uzinduzi huo uliofanyika leo Septemba 13, 2025 kwa shamrashamra kubwa, umehudhuriwa na wananchi, wanachama wa CCM, wagombea wa nafasi mbalimbali akiwemo Mhe. Richard Luhende anayewania udiwani Kata ya Didia, wagombea waliopita kura za maoni, na viongozi wa chama, huku Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mhe. Munde Tambwe Abdallah, akiwa mgeni rasmi.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhandisi Malunde amewahimiza wananchi wa Itwangi kumpa miaka mitano mingine Rais Samia, akibainisha kuwa ndiye aliridhia kuundwa kwa Jimbo jipya la Itwangi baada ya kutengwa kutoka Jimbo la Solwa.

“Nimeisoma Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa Mkoa wa Shinyanga – imesheheni ahadi nyingi za kutatua changamoto za wananchi wa Itwangi kwenye sekta za afya, elimu, miundombinu, kilimo na umwagiliaji,” amesema.

Aidha, amempongeza Rais Samia kwa kuendeleza miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR, akisema Tanzania sasa ni miongoni mwa nchi sita barani Afrika kati ya 54 zenye reli ya kiwango cha juu cha aina hiyo, jambo linalochochea uchumi wa Taifa.

Mhandisi Malunde amewaomba wananchi kumpigia kura Dkt. Samia, Mhe. Azza Hillal na madiwani wote wa CCM ili utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa kipindi cha 2025-2030 usikwame kutokana na changamoto za kisiasa.

Aidha amesisitiza kuwa licha ya kushika nafasi ya tatu katika kura za maoni za ubunge, ameamua kumuunga mkono kwa dhati Mhe. Azza Hillal Hamad baada ya kushinda na kupewa ridhaa ya CCM kupitia vikao vya juu vya chama.

 Aliyekuwa Mtia Nia ya Ubunge Jimbo la Itwangi Mhandisi Sebastian Malunde , akiwaombea kura wagombea wa CCM kwenye  uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Itwangi

Aliyekuwa Mtia Nia ya Ubunge Jimbo la Itwangi Mhandisi Sebastian Malunde , akiwaombea kura wagombea wa CCM kwenye  uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Itwangi

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Munde Tambwe Abdalla akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Itwangi

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Munde Tambwe Abdalla akiwanadi na kuwaombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad (kulia)na Mgombea Udiwani Kata ya Didia Richard Luhende.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464