` HAYA SIYO MAPENZI NI MAHABA MAKUBWA WANANCHI WA ITWANGI KWA AZZA HILLAL HAMAD UZINDUZI WA KAMPENI

HAYA SIYO MAPENZI NI MAHABA MAKUBWA WANANCHI WA ITWANGI KWA AZZA HILLAL HAMAD UZINDUZI WA KAMPENI


Na Marco Maduhu,SHINYANGA

WANANCHI wa Jimbo la Itwangi,wamejitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa kampeni wa jimbo hilo,huku wakionyesha Mahaba makubwa kwa Mgombea Ubunge Azza Hillal Hamad, kuwa wanaimani naye katika kuwaletea maendeleo.

Uzinduzi wa kampeni hizo umefanyika leo Septemba 13,2025 na kuhudhuriwa na wananchi,wana CCM pamoja na Wagombea Udiwani katika Jimbo la Itwangi,huku Mgeni Rasmi akiwa ni MNEC Munde Tambwe Abdalla.
Munde, akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni hizo, amesema wananchi wa Itwangi wamepata Mbunge Jembe sababu ana uwezo mkubwa wa kuwatumikia na kuwaletea maendeleo.

Amesema,anamfahamu Azza tangu alipokuwa Mbunge wa Vitimaalum juu ya utendaji wake kazi kwa kuwasemea wananchi,na hivyo kuwataka wananchi wa Itwangi wamchague awe Mbunge wao siku ya Uchaguzi Oktoba 29 ili awatumikie na kuwaletea maendeleo.
"Azza ni chaguo sahihi kupitishwa kugombea Ubunge katika Jimbo hili la Itwangi,wana Itwangi mmepata Mbunge Jembe kwanza Jasiri, mjenga hoja na mtetezi wa wananchi," amesema Munde.

"Nawaomba wananchi wa Itwangi siku ya kupiga kura Oktoba 29 mpigieni kura za ushindi Mgombea Urais,Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,Azza Hillal Hamad na Madiwani wote wa CCM ili wawaletee maendeleo,"ameongeza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo,amemwagia sifa Azza kuwa ni mchapakazi na mwenye uchu wa maendeleo na kwamba CCM imeweka wagombea ambao wazuri ambao wanauzika kwa wananchi.


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Edward Ngelela,amesema wanaimani na Azza,sababu wanafahamu utendaji wake kazi.
Mbunge Mteule wa Vitimaalum mkoa wa Shinyanga Christina Mzanva naye amemoumbea kura Azza,Rais Dk,Samia pamoja na Madiwani wote wa CCM.

Naye Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad kupitia CCM, akinadi sera kwa wananchi,amesema Itwangi ya maendeleo inakuja na kwamba hakuna Chama ambacho kinaweza kuwaletea maendeleo wananchi zaidi ya CCM.
Amesema,kuna baadhi ya miradi ya maendeleo bado haijakalimika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi zikiwamo Zahanati,kwamba akipata ridhaa ya kuwa Mbunge atazipambania na kuzikamilisha.

Amesema, pia katika Jimbo la Itwangi shughuli kubwa za wananchi ni Kilimo cha Mpunga, na kwamba kuna miradi ya umwangiliaji bado haijakamilika kujengwa ikiwamo Skimu ya Nyida, kwamba atapambana kuikamilisha
Amesema kwa upande wa miradi ya maji,kuwa kuna mradi mkubwa wa maji ya ziwa Victoria na kwamba vijiji vyote ambavyo vinapitiwa na mradi huo atapambania vipate maji, pamoja na vijiji 22 ambavyo vinapitiwa na mradi wa maji Tinde Package.

"Wananchi wa Itwangi Oktoba 29 nikopesheni Imani,niwatumikie katika kuwaletea maendeleo,"amesema Azza.

Pia,Azza amewaomba wananchi wa Itwangi wampigie kura nyingi za ushindi Mgombea Urais,Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, pamoja na madiwani wote wa CCM,ili CCM ishinde na kuwaletea maendeleo.

Amemuelezea Rais Samia,kuwa katika utendaji wake kazi ndani ya miaka mitano,kwamba katika Jimbo la Itwangi ametekeleza miradi mingi ya maendeleo ikiwamo miradi ya kimkakati,na kutolewa mfano mradi wa Reli ya kisasa(SGR) ambayo inapita jimboni humo,kwama itakuwa kichocheo kikubwa cha uchumi.

Ameongeza kuwa Rais Dk.Samia amejenga pia miradi mingine ya maendeleo ikiwamo ya sekta ya Elimu,Afya,Miundombinu ya barabara, na ujenzi wa Skimu za Umwagiliaji.

Nao baadhi ya wananchi wa Itwangi, ameeleza kwamba wanaimani na Mgombea Ubunge Azza,sababu wanamfahamu juu ya utendaji wake kazi katika kutetea maslahi ya wananchi na kuwaletea maendeleo,tangu alipokuwa Mbunge wa Vitimaalum.

Oktoba 29 na Uchaguzi Mkuu wa kuchagua Madiwani,Wabunge na Rais na sasa vyama vya siasa vipo kwenye kampeni za kunadi sera zao kwa wananchi.

TAZAMA PICHA👇👇
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Munde Tambwe Abdalla akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni.


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Munde Tambwe Abdalla akiwa Nadi na kuwaombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad (kulia)na Mgombea Udiwani Kata ya Didia Richard Luhende.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza kwenye mkutano wa kampeni.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akimuombea Mgombea Urais wa CCM,Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad na Madiwani wote wa CCM.
Mbunge Mteule wa Vitimaalum mkoa wa Shinyanga Christina Mzamva akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni.
Mgombea Ubunge wa Vitimaalum Mkoa wa Shinyanga Christina Mzamva akiomba kura za Rais.Dk Samia Suluhu Hassan, na Mgombea Ubunge Jimbo la Itwangi Azza Hillal Hamad na Madiwani wote wa CCM.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akinadi sera kwa wananchi.
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Itwangi CCM Azza Hillal Hamad akiomba kura za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,na kujiombea kura yeye mwenyewe,pamoja na madiwani wote wa CCM.








Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464