` FADHILI NAFUTARI : KAZI NI MOJA TU OKTOBA 29! KUTIKI KWA AZZA HILLAL, DKT. SAMIA

FADHILI NAFUTARI : KAZI NI MOJA TU OKTOBA 29! KUTIKI KWA AZZA HILLAL, DKT. SAMIA

Aliyekuwa mtia nia wa ubunge Jimbo la Itwangi, Fadhil Nafutari Solomon akimuombea kura Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hilal Hamad, Madiwani wa CCM 

pamoja na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan 

Aliyekuwa mtia nia wa ubunge Jimbo la Itwangi, Fadhili Nafutari  akimuombea kura Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hilal Hamad, Madiwani wa CCM 
pamoja na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.Picha na Kadama Malunde
Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mkuu Jimbo la Itwangi mkoani Shinyanga 

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Mwanasiasa Machachari na Kada wa CCM aliyekuwa mtia nia wa ubunge Jimbo la Itwangi, Fadhili Nafutari, ameonyesha mshikamano na ari ya kipekee kwa kutangaza utayari wake wa kuungana na Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hilal Hamad, pamoja na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhakikisha kura nyingi zinakusanywa katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akihutubia maelfu ya wananchi waliofurika katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM Jimbo la Itwangi uliofanyika  Septemba 13,2025 katika Mji wa Didia, Fadhil alisema:
“Nani kama Azza Hillal Hamad? Nani kama Dkt. Samia Suluhu Hassan? Tarehe 29,2025 kazi yetu ni moja tu, ni Kutiki, Kutiki, Kutiki tu kwa Mgombea Urais wa CCM, Mbunge wa CCM na Madiwani wa CCM. Tuna furaha kubwa kwa kazi kubwa zinazofanywa na Mama yetu Dkt. Samia Suluhu Hassan. Sisi wana Itwangi tupo hapa kwa ajili ya kumlipa kwa mambo mazuri aliyoyafanya kuwaletea maendeleo wananchi. Nipo tayari kuungana na Dkt. Samia, kuungana na Azza Hillal Hamad na madiwani wa CCM kwa ajili ya kukusanya kura nyingi sana”.

Katika mkutano huo uliopambwa na shamrashamra za kijani na njano, viongozi mbalimbali wa chama walihimiza mshikamano na mshikikano wa wana-CCM kuhakikisha ushindi wa kishindo.

Simon Mayengo, mlezi wa Jimbo la Itwangi, alisema wananchi hawana shaka na wagombea wa CCM kwa sababu wana sifa zote za uongozi.

“Kama Mlezi wa Jimbo la Itwangi, tunamshukuru sana Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa kutuletea mgombea wetu makini ambaye ni mbobevu katika nafasi hii. Alipumzika kidogo na sasa anarudi kuleta maendeleo ya Jimbo jipya la Itwangi. Oktoba tunatiki kwa Azza Hillal Hamad, Dkt. Samia Suluhu Hassan na madiwani wa CCM,” alisema Mayengo.

Kwa upande wake, Mhe. Azza Hilal Hamad, mgombea ubunge wa CCM Itwangi, aliwaahidi wananchi maendeleo makubwa endapo atapewa ridhaa ya kuwaongoza. Alitaja miradi ya maji, afya, elimu na umwagiliaji kuwa kipaumbele chake, akibainisha kukamilisha skimu za umwagiliaji ikiwemo Nyida na miradi ya maji kutoka Ziwa Victoria na Tinde Package ili vijiji vyote vipate huduma.

“Wananchi wa Itwangi, Oktoba 29 nikopesheni imani niwatumikie. Hakuna chama kingine kinachoweza kuwaletea maendeleo zaidi ya CCM,” alisema Azza, huku akimpongeza Rais Samia kwa miradi mikubwa ya kimkakati iliyotekelezwa Itwangi, ikiwamo reli ya kisasa (SGR), miundombinu ya barabara, elimu, afya na umwagiliaji.

Mgeni rasmi wa uzinduzi huo, Munde Tambwe Abdallah, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), alimwelezea Azza kama “mbunge jembe” mwenye uwezo mkubwa wa kuwatumikia wananchi:

“Azza ni chaguo sahihi. Ni jasiri, mjenga hoja na mtetezi wa wananchi. Nawaomba Oktoba 29 mpigie kura Rais Dkt. Samia, Azza Hillal na madiwani wote wa CCM ili tuendelee kupata maendeleo,” alisema Munde.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na wananchi kwa wingi, wanachama wa CCM, wagombea udiwani na viongozi mbalimbali wa chama, na kuashiria mwanzo wa kampeni za kishindo kuelekea Oktoba 29.
Aliyekuwa mtia nia wa ubunge Jimbo la Itwangi, Fadhil Nafutari Solomon akimuombea kura Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hilal Hamad, Madiwani wa CCM 
pamoja na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Aliyekuwa mtia nia wa ubunge Jimbo la Itwangi, Fadhil Nafutari Solomon akimuombea kura Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Itwangi, Mhe. Azza Hilal Hamad, Madiwani wa CCM 
pamoja na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Munde Tambwe Abdalla akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Itwangi
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Munde Tambwe Abdalla akizungumza kwenye uzinduzi wa Kampeni Jimbo la Itwangi


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464