` MKOKO:WAANDISHI WA HABARI ZINGATIENI MWONGOZO KURIPOTI HABARI ZA UCHAGUZI

MKOKO:WAANDISHI WA HABARI ZINGATIENI MWONGOZO KURIPOTI HABARI ZA UCHAGUZI

Waandishi wa habari wametakiwa kuzingatia mwongozo kuripoti habari za uchaguzi

Na Marco Maduhu,MWANZA

WAANDISHI wa Habari nchini, wametakiwa kuzingatia Mwongozo wa Uandishi wa habari,katika kuripoti habari za uchaguzi, ili kuepuka kuleta taharuki kwa jamii.

Hayo yamebainisha leo Agosti 7,2025, na Dk.Egbert Mkoko kwenye Semina ya Waandishi wa Habari Kanda ya Ziwa na Jeshi la Polisi, wakati akiwasilisha Mada ya Mwongozo wa Waandishi wa habari.

Amesema, lengo la Mwongozo huo ni kuweka misingi ya kitaaluma, kimaadili,usawa,uwazi,weledi,kuchapisha taarifa za kweli na sahihi, kuepuka maudhui yenye kuleta chuki, ubuguzi,kashfa chuki na matusi.

"Mwongozo huu kwa vyombo vya habari, ni kuchapisha taarifa za kweli,sahihi, na zilizoweza thibitishwa na kuhakikiwa kikamilifu ili kuripoti habari za uchaguzi Mkuu kwa usahihi,"amesema Mkoko.
Picha na Malunde 1Blog.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464