NTOBI ATINGA INEC KUCHUKUA FOMU KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI KUPITIA ACT-WAZALENDO
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
Emmanuel Ntobi amechukua fomu za uteuzi kugombea Ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama cha ACT-Wazalendo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025.
Ntobi alichukua fomu hizo leo katika Ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) Manispaa ya Shinyanga, na kukabidhiwa na msimamizi wa uchaguzi wa manispaa hiyo Ally Mohamed, huku akiambatana na baadhi ya viongozi wa chama hicho.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Ntobi amesema dhamira yake ni kuibadilisha Shinyanga kuwa na kasi ya maendeleo, ikiwamo ujenzi wa stendi mpya ya mabasi, barabara za lami, na vituo vya afya kila kata.
Amesema atapigania kubadilishwa sera ya mikopo ya vijana wanawake na watu wenye ulemavu kutoka asilimia 10 hadi kufikia asilimia 40, pamoja na kuondoa tozo na kodi ya huduma (Service Levy) ambazo zimekuwa kero kwa wafanyabiashara.
Kadhalika, amesema atapambania ajira kwa vijana, upatikana kwa chuo kikuu, na ujenzi wa viwanda vitakavyoongeza mzunguko wa fedha na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika mji huo.
TAZAMA PICHA👇👇
Emmanuel Ntobi (kulia)akichukua Fomu za Uteuzi kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia ACT-Wazalendo (kushoto)ni msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Shinyanga Mjini Ally Mohamed.
Emmanuel Ntobi akionyesha Fomu za Uteuzi kugombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia ACT-Wazalendo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464