Na Suzy Butondo,Shinyanga Press Club blog
Mgombea Mteule wa Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kata ya Mwamalili Manispaa ya Shinyanga James Matinde amechukua fomu ya kugombea nafasi ya udiwani akipeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu 2025.
Matinde alichukua Fomu hizo zilizotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) katika ofisi za kata ya Mwamalili James Matinde huku akisindikizwa na jopo kubwa la wanachama wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Mwamalili ameushukuru uongozi wa kata, wilaya na Taifa kwa kurudisha jina lake kwa ajili ya kugombea udiwani kata ya Mwamalili ambapo amesema nafasi hiyo ataiwakilisha vyema na kuhakikisha ushindi wa CCM unapatikana.
Matinde pia amewashukuru wanachama wote wa kata ya Mwamalili kwa kumpatia nafasi hiyo baada ya kushinda kwenye kura za maoni ndani ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kujitokeza kwa wingi kumsindikiza kurudisha fomu.
"Nawashukuru sana wanaCCM wote wa kata ya Mwamalili kwa kuniwezesha kupata nafasi hii ya kupeperusha bendera ya CCM, hivyo nawaahidi kwamba sitawaangusha nitahakikisha ushindi wa kishindo unapatikana kwa Rais, mbunge na diwani, kwa sababu tumefanya kazi kubwa na zinaonekana, hivyo tutaendeleza tena pale tulipoishia", amesema Matinde.
"Niwaombe tu ndugu zangu tuendelee kushirikiana tuwe na upendo pamoja na umoja ili tuweze kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa 2025 ili tupate ushindi wa kishindo", ameongeza.
Kwa upande wake mtendaji wa kata ya Mwamalili Maico Joshua amesema amemkabidhi fomu hiyo ili akajjaze na kurudisha tarehe 27/8/2025
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464
















