MWENGE WA UHURU WAKOSHWA NA MIRADI YA MAENDELEO WILAYANI KISHAPU
Na Marco Maduhu,KISHAPU
MWENGE wa Uhuru umekimbizwa wilayani kishapu,na kumulika miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya sh.bilioni 1.9.
Umekimbizwa leo Agosti 8,2025 na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi na uwekaji wa mawe ya msingi kwenye miradi hiyo,ameeleza kufurahishwa na utekelezaji wake, akiipongeza wilaya hiyo kwa kusimamia kwa ufanisi miradi yenye tija kwa jamii.
"Miradi hii ya maendeleo inagusa maisha ya wananchi,na nimeikagua na kupitia nyaraka zake haina ubabaishaji na imetekelezwa kwa kiwango bora kabisa, fedha za Rais Samia Suluhu Hassan mmezitendea haki," amesema Ussi.
Aidha, amewapongeza wawekezaji wazawa wa Kituo cha Mafuta Bin Salum wilayani humo,na kwamba wameonyesha uzalendo wa hali ya juu,pamoja na kutoa ajira.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi, awali akizungumza mara baada ya kuupokea Mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro amesema Mwenge ukiwa wilayani utamulika miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya sh.bilioni 1.9.
Aidha,miradi iliyo mulikwa na Mwenge wa Uhuru wilayani Kishapu ni Kilimo ha Nyanya,Secondari mpya ya Msagala,mradi wa Maji Ng'wanh'olo,Zahanati ya Wela,Bweni la Wasicha Sekondari ya Mwashele,klabu ya wapinga Rushwa,Barabara ya Lami, na Kituo cha Mafuta cha Bin Salim
Mwenge huo kesho utakabidhiwa Mkoani Simiyu, ukiwa na kauli mbiu isemayo "Jitokeze kushiriki uchaguzi wa mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464