MWENGE WA UHURU WARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MRADI WA MAJI NYENZE,NG'WANGH'OLO
Na Marco Maduhu,KISHAPU
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi,ameeleza kuridhishwa na utekelezaji wa mradi wa maji Nyenze na Ng'wangh'olo wilayani Kishapu.
Amebainisha hayo leo Agost 8,2025 wakati akizindua mradi huo wa maji ambayo ni ya Ziwa Victoria.
Amesema wameukagua mradi huo pamoja na kupitia nyaraka zote kwamba upo vizuri hauna ubabaishaji na umetekelezwa kwa kiwango cha juu na chenye ubora.
"Nawapongeza RUWASA kwa kazi kubwa ambayo manifanya ya kusambaza huduma ya maji vijijini na kuwaondolea changamoto ya ukosefu wa maji, na mimi kama kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru nipo tayari kuuzindua," amesema Ussi.
Aidha, amempongeza Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Shinyanga Julieth Payovela na Mameja wote wa Ruwasa ngazi ya wilaya kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya ya kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan kumtua ndoo kichwani Mwanamke.
Naye Meneja wa RUWASA Wilaya ya Kishapu Mhandisi Dickson Kamazima, amesema mradi huo ulianza kujengwa Februari 2024 na kukamilka Agosti mwaka huo,kwa gharama ya sh.milioni 445.
Amesema, mradi huo unanufaisha wananchi 2,345 wa vijiji hivyo vya Nyenze na Ng'wanh'olo.
Nao baadhi ya wananchi wa vijiji hivyo,kwa nyakati tofauti wamesema,mradi huo wa maji umekuwa mkombozi, kwao kwa kuondokana na adha ya ukosefu wa maji safi na salama.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru Mwaka huu inasema"Jitokeze kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.
TAZAMA PICHA👇👇👇
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2025 Ismail Ali Ussi akikata utepe kuzindua mradi wa maji