Mwenge wa uhuru kumulika mradi 7 ya maendeleo ya bilioni 1.9 Kishapu
Na Marco Maduhu,KISHAPU
Mwenge wa Uhuru katika wilaya ya Kishapu utamulika miradi 7 ya maendeleo yenye thamani ya sh.bilini 1.9.
Mwenge wa huo wa Uhuru umewasili leo Agost 8,2025 wilayani Kishapu ukitokea Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Peter Masindi akizungumza mara baada ya kuupokea Mwenge huo, kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Peter Masindi,amesema ukiwa wilayani Kishapu utazindua,kuona na kuweka mawe ya msingi miradi 7 ya maendeleo ya sh.bilioni 1.9.
Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru,zinaongozwa na kiongozi wake Ismail Ali Ussi.
Na Kauli Mbiu ya Mwaka huu ya Mwenge wa Uhuru inasema"jitokeze kushiriki uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu.