
DORINA PETER OKANGA AMECHUKUA FOMU KUWANIA UBUNGE KUNDI LA VIJANA TAIFA
Dorina ambye ni mjumbe wa mkutano mkuu Taifa UVCCM TAifa ambaye pia ni mwenyekiti wa SMAUJATA wilaya ya Kahama leo amechukua fomu ya kuwania Ubunge kupitia kundi la vijana Taifa ili kuwawakilisha vijana wenzake.
Dorina ambaye pia ni muuguzi katika hospital ya manispaa ya Kahama amesema ameamua kuwania nafasi hiyo ili kuwawakilisha vijana wenzake Bungeni,kuwasemea changamoto mbalimbali wanazozipitia.
"Kwa vile ni natoka kwenye utumishi pia watumishi wenzangu nitaenda kuwasemea huko bungeni na nitakuwa mwakilishi wao, kuwasemea changamoto zote walizonazo"amesema Drina.


Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464