
Na Suzy Butondo, Shinyanga
Alice aahidi kufanya makubwa kwa wanawake wa mkoa wa Shinyanga endapo atafanikiwa kuwa mbunge wa viti maalum
Mgombea ubunge viti maalum Alice Salvatory Kyanila ameweka wazi vipaumbele vyake endapo akipata nafasi ya Ubunge, amesema ana vipaumbe vitatu vya kuwasaidia kina mama wa mkoa wa Shinyanga.
Alice amesema kutokana na yeye kufanikiwa mpaka kufikia kuitwa Malkia wa madini ni kutokana na kufanya juhudi kubwa za kuwatembelea kina mama wote wanaoshughulika na shughuli za uchimbaji na kuweza kupata vifaa vya kufanyia kazi.
"Hivyo nimepata chachu kubwa sana kwamba nikitumia njia hii inaweza kuwaambukiza kina mama wa Shinyanga waweze kujua ni namna gani wanaweza kutunisha mifuko yao kwa kutumia ujasiliamali mdogo mdogo wa kuongeza vipato katika familia zao na kwa Taifa kwa ujumla"amesema Alice.
Kipaumbele cha kwanza ameona wanawake wanaweza kufanya ufugaji wa kuku wa kisasa kutokana na mkoa wa Shinyanga kuwa na joto, wanaweza kustahimili kufuga kuku wa mwezi mmoja na chotala wa miezi mitatu pia anaweza kuleta mashine za kutotolesha vifaranga ambapo ataanza na watu saba waliomo ndani ya chama na baada vikundi vingine.
"Watu hao saba ambao watakuwa kikundi wakishirikiana kufuga vifaranga watazalisha na kuweza kuwagawia wengine, kama mtu ana uwezo wakufuga kuku 10 au saba huyu mtu anaweza kufuga kuku 100 na vikatoka vikawa salama, hivyo nitaleta maafisa wagani ambao watawajengea uwezo,"amesema Alice.
"Kuna wengine watahitaji kufanya biashara ya kilimo tutaongeza tija katika uzalishaji,ntajitahidi kutafuta mashine kama Power tiler kwa wadau mbalimbali za ruzuku ili wakulima waweze kujipatia kipato, lakini kwa wale ambao hawahitaji kulima hata kufuga tutawafundisha ni namna gani wataweza kuzalisha wadudu ama minyoo kwa ajili ya kujipatia kipato,"aneongeza.
Amesema baada ya kuletwa vifaa hivyo watafundishwa ni namna gani ya kutengeneza wadudu hao mabaki ya nyumbani yote unayatunza na kuweza kutengeneza chakula cha kuku.
"Pia tunakiwanda cha jambo hapa Shinyanga ambacho kinaweza kusaidia kina mama kujipatia kipato kwa kupeleka maziwa katika kiwanda hicho, kutokana na familia nyingi kuwa na Ng"ombe "hivyo Jambo ana mpango mzuri wa kukusanya maziwa kwa ajili ya kutengeneza maziwa hayo, na hili nitalisimamia mwenyewe "amesema Alice