` RC MBONI AMUAPISHA DC MPYA WA KAHAMA FRANK NKINDA

RC MBONI AMUAPISHA DC MPYA WA KAHAMA FRANK NKINDA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita,amemuapisha Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank John Mkinda,mara baada ya kuteuliwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa wilaya hiyo.
Amemuapisha leo Julai 1,2025 kwenye ukumbi wa mikutano katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga,hafla iliyohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali,Chama na Taasisi mbalimbali za Serikali, viongozi wa dini na kimila.

Mboni akizungumza mara baada ya kumaliza kumuapisha DC Nkinda,amemuahidi kumpatia ushirikiano wa kutosha sababu Kahama anaifahamu vizuri na kwamba kabla ya kupanda kuwa Mkuu wa Mkoa,alikuwa Mkuu wa wilaya hiyo.
“Nakupongeza kwa kuaminiwa na Rais Samia na kuteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Kahama,mimi nipo na nitakupatia ushirikiano wa kutosha,”amesema Mboni.

Aidha,ametoa maagizo kwa Wakuu wa wilaya wote wa Mkoa huo, kwamba waendelee kudumisha Amani na utulivu katika maeneo yao,pamoja na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.
Pia,amewaagiza kuendelea kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na ukamilishaji wa maboma ya Zahanati kwa kutumia mapato ya ndani,ili kusogeza huduma kwa wananchi.

Amewasisitiza kutafuta wawekezaji, ili kuwepo na mzunguko wa fedha katika maeneo yao na kuinua uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.
Ameagiza pia kusimamiwa kwa Zao la Pamba,pamoja na Kongani la Biashara”Buzwagi Special Econoc Zone”kwa upande wa Kahama,lengo ikiwa ni kurudisha mzunguko wa kifedha,kama awali wakati Mgodi wa Buzwagi ukifanya kazi kabla ya kufungwa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,amemkaribisha Mkuu huyo mpya wa wilaya ya Kahama, na kuahidi watampatia ushirikiano.

Naye Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Mkinda,ameahidi kutekeleza maagizo yote aliyopewa,huku akiahidi kudumisha Amani na Utulivu katika wilaya hiyo, hasa kwenye kipindi hiki cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu 2025.

TAZAMA PICHA👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga CP Salum Hamduni akizungumza.
Mkuu wa wilaya mpya wa Kahama Frank John Nkinda akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akimuapisha Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank John Nkinda.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464