` SOPHIA MSELEMU KAZIMIL ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE KUPITIA JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA

SOPHIA MSELEMU KAZIMIL ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE KUPITIA JUMUIYA YA WAZAZI TAIFA


Na Suzy Butondo,Shinyanga

SOPHIA MSELEMU KAZIMIL ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE KUPITIA JUMUIYA YA WAZAZI

"Ninagombea viti maalum kwa sababu nina wito wa dhati wa kuwatumikia wananchi, hasa katika eneo la malezi na maendeleo ya watoto na familia"anaeleza Sophia

"Kama mwalimu mwenye uzoefu wa muda mrefu, nimeona kwa karibu changamoto zinazowakabili watoto wetu, wazazi na walimu katika jamii. Kupitia taaluma yangu ya ualimu,nimejifunza kuwa msingi wa taifa bora ni malezi
bora"

"Naamini kuwa kwa nafasi ya uongozi, ninaweza kuwa sauti ya wazazi na walezi,kusukuma mbele sera zinazoweka mazingira rafiki kwa mtoto, shule salama na jamii inayojali
maadili.

"Ninataka kutumia nafasi hii kuhamasisha sera za elimu jumuishi, ulinzi wa mtoto, na uwezeshaji wa wazazi ili waweze kulea kizazi
cha kesho chenye maadili, maarifa, na
uzalendo,

"Hii siyo tu ndoto yangu kama
mwanamke na mzazi, bali pia kama mwalimu ninayetambua thamani ya kuwekeza kwenye malezi ya mtoto kwa maendeleo ya taifa zima"Ameeleza Sophia.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464