` FAHAD MUKADAM AJITOSA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI

FAHAD MUKADAM AJITOSA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI

Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Fada Gulamhafiz Mukadam,amechukua Fomu ya kuomba Ridhaa ya Chama chake kumteuwa Kugombea Ubunge katika Jimbo la Shinyanga Mjini.

Amechukua Fomu hiyo leo Julai 2,2025 katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Mjini

Akizungumza mara baada ya kuchukua fom, amesema ameamua kutumia haki yake ya kikatiba na ya msingi kama mwanachama wa CCM mwenye sifa stahiki, ili kuchangia maendeleo ya wananchi wa Shinyanga kupitia nafasi ya ubunge.

"Mimi ni mtoto wa Shinyanga. Nimechukua fomu kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi kugombea ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini. Kama ilivyo taratibu za chama chetu, kila mwenye sifa ana haki ya kugombea. Nimetumia haki yangu ya kikatiba na natamani kushirikiana na wana Shinyanga kuleta maendeleo," amesema Fahad.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464